RC Makonda aliwasili bungeni na kupokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari-Bunge, Owen Mwandumbya kuitikia wito wa Kamati ya Bunge.
 |
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam akisindikizwa kupekekwa kwenye kamati ya Bunge na Owen Mwandumbya kuelekea kwenye mahojiano mapema hapo jana. |
MKUU wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda leo Machi 29, amebanwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo hivi punde ameanza kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Makonda akihojiwa na Kamati ya Bunge Mjini Dodoma.
Hatua hiyo ya kumita RC Makonda kujibu tuhuma zinazomkabili ilifikiwa bungeni wiki chache zilizopita baada ya kuafikiwa kwa hoja iliyotolewa bungeni na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge.
Pia Mwita alidai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.