0
Mkutano mkuu wa chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha Tumaini (TUMAINI SACCOS) kimefanyika jijini Arusha ikiwa ni mkutano wa 27 wa chama hicho tangu kilichoanzishwa mwaka 1990 kikiwa kimekusanya wafanyakazi wa mashirika mawili yasiyo ya kiserikali ya World Vision, Vision Fund na wafanyakazi wa Tumaini  Saccos wakati mpaka sasa kina wanachama wapatao 758 ambao kwa pamoja wanaunda chama hicho cha wa Tumaini Saccos wakiwa ni waajiliwa kutoka mashirika hayo mawili.

Viongozi waandamizi wa Tumaini Saccos wakiongozwa na Mwenyekiti Neema Fredrick (katikati, aliyeshika kipaza saauti) wakiwa katika meza kuu kwa ajili ya kuendesha mkutano mkuu wa chama leo jijini Arusha.

Baadhi ya wanachama kutoka kushoto; Joyce Mallya, Alice na Sia wakifuatilia
 muhtasari wa mkutano mkuu wa mwaka 2017 jijini Arusha.
Emmanuel Sanka akiongea na wanahabari juu ya Tumaini Saccos kilivyofanikiwa katika utendaji wake kwa miaka takribani 27 kwenye
tasnia ya mikopo kwa wanachama wake.
Baadhi ya wanachama wakiwa makini kufuatilia majadiliano ya
Mkutano mkuu wa mwaka 2017 jini Arusha.


Mwenyekiti Tumaini Saccos Neema Fredrick akiongea huku afisa ushirika wa jiji la Arusha (kushoto) Winston Nsemwa akiwa makini kusikiliza na Meneja wa Chama Zawadi Bella (kulia) meneja akiandika kinachojiri

Wanachama wa chama cha Tumaini Saccos wakiwa katika mkutano
mkuu wa chama katika mkutano wa 27 wa chama chao uliofanyika
katika ukumbi wa Corridor Spring Hoteli jijini Arusha.


ARUSHA.
Akiongea katika ufunguzi wa mkutano huo mkuu wa chama Mrajisi msaidizi wa vyama vya akiba na mikopo mkoa wa Arusha Emmanuel Sanka  amesema kuwa wakati kukiwa na matatizo kadhaa kwenye baadhi ya vyama vya akiba na mikopo si kazi raisi kwa saccos kuandaa mkutano mkuu wa mwaka kama walivyofanya Tumaini Saccos lakini ili linatokana na uongozi madhubuti unaokuwepo.

“Mimi nawapongeza sana kwa hatua hii kwa sababu vyama vingine vya Akiba na mikopo wanashindwa kuandaa mkutano mkuu wa mwaka kutokana na sababu zisizofahamika, lakini niseme jambo moja hapa, wakati kuna walakini kwenye baadhi ya taarifa za Saccos nyingine, imepelekea mrajisi wa vyama vya ushirika ameunda tume ili kuchunguza mapungufu yaliyopo hasa ya upotevu wa pesa za watu, hakuna mtu anayependa kuona fedha ya mtu inapotea lakini tunaangalia kuona ni namna gani fedha za watu zinalejeshwa” Alisema Emmanuel.

Wakati chama kumekuwa na ogezeko utoaji wa mikopo kwa mwaka 2015/16 kwa wastani wa shs 3,291,173,663bilioni ambapo kiutekelezaji, utoaji huo unaonyesha kuvuka lengo la bajeti kwa asilimia 46%.

Wakati malengo makubwa ya chama hicho ni kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wanachama, Mwenyekiti wa chama cha Tumaini Saccos Neema Fredrick anasema chama hicho kina mtaji usiopungua 6bilioni ambazo zinatumika kufanya uwekezaji pamoja na kutoa mikopo kwa wanachama, ikiwa ni pamoja na kuwa na mfuko wa kijamii unaohudumia wananchama wanapokumbwa na matatizo ya kijamii kama misiba.


“Urejeshwaji wa mikopo kutokana na tatizo la uchumi kwa baadhi ya wanachama sisi Tuamaini Saccos bado tupo kwenye hali nzuri kutokana portfolio ya Tumaini ni 2% kwani taasisi zinazofanya huduma ya mikopo kwa watu zinasema isizidi 5%, kwa hivyo tupo kwenye hali nzuri ya urejeshaji wa mikopo, lakini waajili wa mashirika haya mawili World Vision na Vision Fund wanatusaidia kukata mikopo kutoka kwenye mishahara yao kabla haijapelekwa benki hivyo tuna nafasi nzuri kwa upande huo” Anasema Neema.











Post a Comment

 
Top