0
 PROFILE PHOTO: 
Dar Es Salaam Regional Commissioner Paul Makonda
Kitendawili cha elimu pamoja na vyeti vya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam imekuwa ni gumzo kwa sasa ikiwa ni kwenye mitandao ya kijamii na mazungumzo ya watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifuatilia jambo hili na ikiwezekana wengine wakitaka kujua kulikoni.


DAR ES SALAAM.
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni sawa ziendelee kwani ni dalili kwamba vita dhidi ya dawa ya kulevya imefanikiwa.

Makonda amesema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twende zetu Kigamboni jiji Dar Es Salaam lililofanyika katika wilaya hiyo ambapo alisema mapambano ya dawa za kulevya ni ya kupona au kufa.

“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka” alisema Makonda.

Dar Es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kipo katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelelenyingi kama ambavyo zinaendelea sasa, aliongeza Makonda.

“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dawa za kulevya si rahisi” Alisema Makonda.





Source Habari Leo.

Post a Comment

 
Top