0
DAR ES SALAAM
Habari za muda huu ni kwamba aliyekuwa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo,  Nape Nnauye alikuwa aongee na vyombo vya habari mchana huu katika hotel ya Protea jijini Dar Es Salaam amezuia na watu wanaosadikika kuwa ni askari waliokuwa wamevalia kiraia.

Katika eneo lililopo karibu na hotel hiyo mbuyuni msasani Nape amelalamika kwa nini wamtolee bastola,  akiwa kwenye gari anayotumia kwa sasa, "Mimi sina kinyongo na uhamuzi wa Rais, kama sikumshawishi kunichagua hata kuniacha ni sawa tu",  alisema Nape Nnauye.


Aitha Nape aliongeza kwa kusema, "Watanzania tuungane kudumisha umoja na mshikamano wa nchi yetu, ninajua kuna watu kwa namna moja hama nyingine wameumia, ninawaomba kama mimi mnayeniamini kuwa mambo yako sawa, maisha lazima yaendelee, tuitulize nchi, hatuna sababu ya kuvurugana".

Akizungumza akiwa juu ya gari land cruiser aliongeza kwa kusema, "Nape ni mdogo kuliko nchi, tusije tukamgeuza nape akawa badala ya Tanzania, Tanzania ni kubwa kuliko Nape hivyo basi ninawaombeni sana,  moyo wangu, nafsi yangu mwili wangu unawapenda sana kwani nilitamani kuendelea kufanya kazi na nyie lakini wakati wa aliyeniweka umefika mimi kuondoka lakini tutaendelea kuwa pamoja".

Mbunge huyo wa Mtama aliwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kumtumia meseji za pole na akubaki nyuma kwani kupitia nafasi hiyo aliwaambia kuwa ataendelea kuwatumikia kwani alipoacha nafasi ya katibu mwenezi wa ccm alienda kuomba ubunhe na siyo uwaziri hivyo atajikita kufanya kazi ambayo wananchibwa jimbo lake ndiyo waliomtuma kwenda kufanya.

"nitawatumikia kwa moyo wangu,  nitapambana kwa maendeleo yako na yale niliyoahidi nitafanya na ninawaombeni sana tutulie, tuendelee na sbuguli zetu" alisema Nape Nanuye. .


Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top