0

PROFILE PHOTO: Rais Yoweli Museveni wa Uganda.

DAR ES SALAAM.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amewasili nchini ikiwa ni ziara ya siku mbili nchini kuanzia leo Jumamosi lengo kuu likiwa kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya Tanzania na Uganda, Museveni anatarajiwa kuwa na mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais Magufuli, pia atatembelea viwanda vya kampuni ya Said Salim Bakhresa ambaye amewekeza pia nchini Uganda.
Aidha rais Museveni atatembelea bandari ya Dar es salaam kujionea utendaji kazi unavyoendelea katika bandari hiyo baada kwa kuwa asilimia kubwa ya mizigo ya nchi hiyo usafirishiwa kupitia bandari ya Mombasa tofauti na hapo awali ambapo bandari ya Dar Es Salaam ndio ilikuwa inasafirisha asilimia kubwa ya mizigo hiyo.
Akizungumza na wanahabari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda Balozi Dkt Augustine Mahiga amesema mambo mengine ambayo yataongelewa katika ziara hiyo ya siku mbili ni hatua ambazo zimepigwa katika ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta gafi kutoka Hoima katika ziwa Albert Uganda hadi bandari ya Tanga.
Bomba hilo ambalo litakuwa na urefu wa km 1442 na kwa upande wa Tanzania peke yake litakuwa na urefu wa Km 1147 na baada ya kufika kwenye bandari ya Tanga ndipo yatasambazwa sehemu mbalimbali duniani na ujenzi wa bomba hilo unatarajia kutoa ajira kwa watanzania wasiopungua elfu kumi.

Post a Comment

 
Top