0
Benki ya First Natinal Bank (FNB) imezindua tawi jipya mkoani Arusha ikiwa ni hatua moja wapo ya kukuza uwekezaji kupitia upande wa fedha,ambapo tawi hilo jipya lilipo katika jengo jipya la PPF Plaza linakuwa ni moja kati ya matawi yake 10 yaliyopo nchini katika kutoa huduma za kifedha.

Naibu waziri wa fedha na mipango Dr.Kijaji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya benki hiyo.

Kushoto mkurugenzi mtenadaji Dave Aitken akiangalia Naibu waziri wa fedha na mipango Dr.Kijaji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya benki hiyo.



Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro akisaini kitabu cha wageni ili kuweka kumbukumbu.


Dr. Kijaji na Dave Aitken wakibadilisha mawazo kabla ya tukio la ufunguzi.


Kikundi cha Sanaa cha wa maasai waliokuwepo kunogesha sherehe za ufunguzi wa tawi hilo jipya kwa kanda ya kaskazini.

Wageni waliofika katika sherehe za ufunguzi wa tawi hilo jipya kwa kanda ya kaskazini, wakipoga picha wamasai (hawapo pichani) kuweka kumbukumbu.

Vijana wa kikundi sarakasi cha jijini Arusha hawakusita kuonyesha ujuzi wa wao katika sarakasi.


Afisa mtendaji wa  benki ya FNB Dave Aitken akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo mkoani Arusha ambapo alisifu uwekezaji huo waliofanya kwa upande wa fedha.

Wafanyakazi wa Benki hiyo kutoka makao makuu Dar Es Salaam na Arusha wakifuatilia matukio katika ufunguzi huo.


Naibu waziri wa fedha na mipango Dr. Ashantu Kijaji akiongea na wageni, wananchi, wafanyakazi waliofika katika ufunguzi wa tawi la Benki ya FNB jijini Arusha ijumaa iliyopita.

Baadhi wageni, wananchi waliofika kuhudhulia ufunguzi huo.

Naibu waziri wa fedha na mipango Dr. Kijaji (katikati) akikata utepe kufungua tawi jipya la Benki ya FNB jijini Arusha, kushoto kwake ni meya wa jiji la Arusha na anayefuatia ni mkurugenzi wa jiji, kulia kwa waziri ni mkuu wa wilaya ya Arusha, anayefutia ni meneja mkuu wa FNB,

Picha inayofuatia wakipiga makofi baada ya kukata utepe.


Meneja wa tawi Edna Kallape akitoa maelezo kwa naibu waziri wa fedha kuhusu utendaji yakinifu kwa kutumia Simu ya kiganjani kutokea kwenye ATM za tawi hilo.

Mtaalam wa Computa wa tawi hilo akitoa maelezo kwa naibu waziri wa fedha Dr. Kijaji kuhusu mawasiliano kutoka benki nyingine kwa kutumia teknolojia iliyopo kwenye tawi hilo.

Naibu waziri Dr, Kijaji kulia akisisitiza jambo kuhsu utendaji unaotakiwa kwa mtoa huduma za wateja wa benko hiyo.


Meneja wa tawi Edna Kallape akitoa maelezo kwa naibu waziri wa fedha kuhusu utendaji yakinifu unaotarajiwa kufanywa katika tawi hilo.


Picha ya wafanyakazi, wageni waalikwa wakiwa pamoja na Mgeni rasmi naibu waziri wa fedha na mipango mara baada ya ufunguzi wa tawi hilo lililopo katika jengo la PPF Plaza barabara ya zamani ya moshi jijini Arusha.



Picha zote na TODAYS PRODUCTION
 +255 757 800 307     




  ARUSHA.
Benki hiyo imekuwa ikifanya kazi zake katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara tangu mwaka 1874 mpaka sasa inatoa huduma katika nchi za Afrika kusini, Tanzania, Lesotho, Namibia, Botswana, Zambia, Msumbuji na Swaziland huku ikiwa na mipango ya kuhudumia watu wengi zaidi barani Afrika.

Akifungua sherehe fupi na kumkaribisha mgeni rasmi Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo nchini Dave Aitken amesema wamefungua tawi hilo mkoani Arusha ili kusambaza huduma ambazo wananchi wanazikosa sehemu nyingine kupitia huduma za kifedha.

“pamoja na kuwepo kwa idadi ya benki zinazokadilia kufika 60, kutokana na hilo kuna changamoto nyingi kuwafikia wateja wengi pamoja na kutoa huduma zinazokidhi matakwa ya mteja moja kwa moja, maana uwekezaji wa fedha unatakiwa kuwafikia wananchi wengi kutokana na maisha ya watu yanagusa fedha kwa muda mwingi” Alisema David Aitken.

Ameendelea kusema kuwa katika tawi hilo lilipo barabara ya zamani ya kuelekea Moshi litakuwa na huduma ya kuweka na kutoa fedha kwa masaa 24 kwa mwaka mzima, pasipo mteja kupitia kaunta ila ataweza kutumia mashine za kisasa za ATM zenye huduma hiyo, “huu ni makakati endelevu unaolenga kuhakikisha maeneo mengi nchini yanapata huduma za kifedha na tawi hili ni kutokana na maslahi ya ukuaji wa haraka wa mkoa wa Arusha ambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi”aliongeza David

Naye naibu waziri wa fedha na mipango Dr. Ashantu Kijaji aliyekuwa mgeni rasmi aliyezindua tawi hilo azindua tawi hilo alisema, mkoa wa Arusha ukiwa ni mmoja kati ya mikoa mikubwa kiuchumi na katika ukuaji katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii, uwekezaji wa fedha kupitia benki ni kiashilia kuwa mji unakuwa kwa kasi.

Dr. Ashantu Kijaji alisema “Arusha ina fulsa na hazina kubwaya rasilimali, jambo linalochangia ukuaji wa haraka wa biashara katika sekta mbalimbali muhimu za kiuchumi, na ni matumaini yetu kama serikali uwepo wa benki hii ya FNB katika jiji hili utachangia katikakuleta maendeleo ya biashara za aina yote zikiwepo ndogondogo, za kati na kubwa kupitia maendeleo na ubunifu wa kibenki”


Tawi la Arusha linakuja na bidhaa zikiwepo huduma mbalimbali zilizobuniwa mahususi kwa ajili ya kuwaongezea tija wateja wa kawaida na wafanyabiashara katika kanda ya kaskazini.




Post a Comment

 
Top