0
PROFILE PHOTO: Rais wa Marekani Donard Trump.
PROFILE PHOTO: Wachawi waliokusanyika usiku kufanya mambo yao.



MAREKANI:
Siku ya Ijumaa majira ya usiku wa manane, Wamarekani wanaoamini uchawi nchini kote Marekani waliandaa matambiko yenye nia ya kumuondoa Trump katika nafasi yake urais,  cha ajabu mpaka sasa ukurasa wa Facebook wa matambiko hayo umepata wafuasi 10,500.
Hatua hiyo imezua ghadhabu kotoka kwa Wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao kwa kutangaza vita vya kiroho, hata hivyo wachawi hao wanapanga kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini/madarakani, ambapo tambiko lingine litafanyika tarehe 26 mwezi ujao/machi.
Wapinzani wengi wa rais wa Marekani Donald Trump wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka minne ili aweze kuondoka madarakani, hata hivyo wachawi nchini Marekani hawakubaliani na hilo na kubaini kwamba bw Trump anapaswa kuondoka madarakani kabla ya muhula wake wa kwanza kumalizika.
Wakati huo huo chama cha Wakiristo nchini humo kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili uchawi huo, rais wa Marekani Donald Trump mpaka sasa hajazungumzia lolote kuhusu mkasa huo.


Source rfi

Post a Comment

 
Top