0
Hivi karibu serikali ilitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendo kasi itakayojengwa kutoka Dar Es Salaam mpaka Morogoro kwa hawamu ya kwanza huku fedha za mradi huo mkubwa zikiwa zinatoka ndani ikiwa ni bajeti ya serikalina siyo mkopo kama wananchi walivyokuwa wanadhani.

PROFILE PHOTO: Haina uhusianao na habari hii.




DAR ES SALAAM.
Wakati wa sherehe ya kumwapisha mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi Ikulu jijini Dar Es Salaam Generali Venance Mabeyo Rais Magufuri alisema, reli hiyo itakayokuwa inatumia umeme itejengwa kwa shilingi za kitanzania 2 trilioni ambazo ni fedha za Watanzania na wala siyo fedha za serikali ya Uturuki kama ambavyo vyombo vya habari kadhaa vililipoti.

Aliongeza kusema kuwa reli hiyo itakayokuwa na umbali wa kilomita 300 itakuwa na njia kuu pamoja na njia za mchepuko kwa ajili ya kubeba mizigo, ambapo amelilinganisha reli hiyo na zile zinazojengwa katika nchi jirani za Kenya na Ethiopia na kusema ni tofauti kutokana na uwezo wa excel yake inauwezo wa kubeba 25 tani wakati hii yetu itakuwa na uwezo wa kubeba 38tani  “reli hii tunapanga kuijenga itakuwa ya kisasa zaidi kwani inatumia umeme, sasa kuna watu wanadhani fedha za ujenzi wa reli hiyo ni za waturuki, hapana ni kwa asilimia 100 ni za serikali”

Vilevile aliweka mkazo kutokana na umuhimu wa reli hiyo huku akitaka rasilimali na nguvu kazi zote za serikali ziweze kutumika ili kuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kutumia rasilimali watu wafungwa, ambapo kutawexza kupunguza garama za ujenzi, aliongeza kwa kuagiza kuwa wafungwa washiriki kwenye ujenzi wa reli hiyo kama nguvu kazi kwa “kuponda kokoto, kusukuma mawe ili wakitoka gerezani wawe safi na wasifanye mabaya tena”

PROFILE PHOTO: Picha ya treni ya Umeme haina uhusianao na habari hii.


Rais alitaka wafungwa wafanye kazi kwa misingi ya uzalishaji na siyo kukaa tu wanakula.

Post a Comment

 
Top