![]() |
Mratibu wa
mkutano huo Mueno Udeozor kutoka nchini kenya akiongea katika mkutano wa
majumuisho ya pamoja uliofanyika katika hotel ya Naura ijini Arusha.
|
![]() |
Wadau wa
kilimo kutoka nchi kadhaa wakimsikiliza Mueni Udeozor (hayupo pichani)
alipokuwa akitoa mada fupi.
|
ARUSHA.
Tabia nchi imekuwa ni
sehemu mojawapo inayofanyiwa mijadira mbalimbali kutokana na mabadiriko
yanayosababishwa na uharibifu w mazingira ambapo maendeleo ya viwanda kwa nchi
zilizoendelea na kwa nchi za dunia ya tatu ukataji wa miti kwa matumizi
mbalimbali kubwa likiwa uchomajo wa mkaa hali hiyo inasababisha ukosefu wa mvua
kunakopelekea ukosefu wa mvua na upungufu wa chakula.
Mkutano wa tano wa
wakulima nchini unaohamasisha ukulima wa kisasa kwa nchi kanda ya Afrika
mashariki unaoegemea katika ukulima ndani ya miaka miwili juu ya njia bora za
kilimo endelevu unaojulikana kama kilimo hifadhi. Shirika holo lilianza kama
benki ya kuhifadho chakula na kukipeleka katika sehemu zenye njaa limeanzisha
mradi huu ili kuwasaidia wananchi kujilinda na mabadiriko ya bali ya hewa
pamoja na ukulima wa kubifadhi.
Katika mkutano huo
ulioshirikisha mataifa zaidi ya 6 za kiafrika ikiwemo nchi ya Canada kupitia
shirika la Canadian Foodgrains Bank ambayo ndiyo muandaaji na msimamizi wa
mkutano huo, umelenga katika kuwasaidia wakulima wa nchi hizo ili kuweza
kujinusuru na uhaba wa chakula unaondelea kuzikumba nchi hizo kutokana na tabia
nchi na mazingira
Kongamano hilo kubwa na
lenye lengo la kuwapa ujuzi wataalmu mbalimbali wakiwemo maofisa kilimo,
wachungaji na watu wengine watakaokuwa karibu ma wananchi utaanza kufanyiwa
kazi nchini Tanzania kwa kuanzia na mikoa ya kanda ya ziwa kama Mara, Shinyanga,
Geita na Mwanza ili ikiwa ni sehemu mojawapo ambapo kunaonekana kuna
uhaba wa mvua na chakula.



Post a Comment