0
Sakata la watu mashuhuri wanaotakiwa kuhojiwa na wengine kujipeleka kituo kikuu cha polisi jiji Dar Es Salaam linaendelea huku tayari viongozi na wafanyabiashara kadhaa wakiwa wamekwenda kituoni hapo, taarifa zpo nyingi lakini kuna hii ya Mbowe nakuletea hapa.
PHOTO PROFILE: Freeman Mbowe MP.

DODOMA.
Kufuatia hatua nyingine mwenyekiti huyo wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma amesema hawezi kwenda polisi kuhojiwa kama alivyoamuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Hata hivyo Mbowe amesema atakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka zinazohusika ikiwa tu utaratibu sahihi utafuatwa katika uchunguzi unaotakiwa, vile vile ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kwa madai ya kumshushia hadhi kama mbunge na kiongozi  mkuu wa upinzani bungeni akihusishwa na tuhuma hizo za dawa haramu za kulevya.

Post a Comment

 
Top