![]() |
PHOTO: Meya wa jiji la Arusha
Karisti Lazaro,
akiongea katika balaza hilo. |
Balaza la madiwani la jiji la Arusha limekaa na
kutathimini maendeleo ya jiji la Arusha pamoja na kupewa tathimini ya miradi
kadhaa ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji, umeme, Sumatra, AICC
ukiwemo ukarabati wa barabara zinazosimamiwa na halmashauri ya jiji la Arusha.
Mkoa wa Arusha ukiwa na tatizo la kukatika mara kwa
mara kwa umeme, shirika la umeme nchini Tanesco kupitia meneja wa ufundi
wa mkoa wa Arusha amesema wapo katika maboresho ya huduma kwa wateja, pia
shirika lipo katika mpango mahususi wa kuwafanya wananchi waweze kupata taarifa
zote za msingi kupitia simu za kiganjani (smartphone), huduma hiyo itawafanya
wananchi kufuatilia na kupata taarifa kwa wakati na muda wote popote walipo.
![]() |
| Kulia: Naibu Meya Viola Lekindikoki, katikati Mstahiki Meya Kalisti na Mkurugenzi wa jiji la Arusha. |
Meneja wa shirika la usimamizi wa vyombo vya usafiri
majini na nchi kavu mkoa wa Arusha Allen Mwani anasema kwa sasa Sumatra wapo
katika upembuzi yakinifu wa kuondoa usafiri wa daladala maarufu, 'hiace'
ambazo hazina viwango katika usafirishaji wa abilia ikiwa na maana arusha ni
jiji hivyo mpango uliopo ni wadau kukaa pamoja na kuleta magari makubwa ya
usafirishaji wa abilia katika jiji la Arusha.
![]() |
| Baadhi ya Madiwani wa jiji la Arusha wakifuatilia majibu ya mameneja na wataalam wa mashirika ya umma walifika kuleta taarifa za miradi. |
![]() |
Wageni kadhaa kutoka
country ya Nairobi waliofika kupata ujuzi na uzoefu wa balaza la madiwani kwa
hapa nchini.
|
![]() |
Madiwani wa jiji la Arusha wakiwa katika kikao kinachofanyoka katika
ukumbi wa jiji kupokea taarifa za miradi kadhaa ya jiji Arusha.
|
![]() |
Wageni kadhaa kutoka
country ya Nairobi waliofika kupata ujuzi na uzoefu wa balaza la madiwani kwa
hapa nchini.
|
![]() |
Madiwani wa jiji la Arusha wakifuatilia majibu ya mkurugenzi juu ya hati ya kiwanja cha mpira wa miguu cha Sheikh Amri Abeid ambacho ni mali ya Chama Cha Mapinduzi -CCM.
|
ARUSHA.
Katika balaza hilo mkurugenzi wa jiji
ameomba gari la wagonjwa lililotolewa na mbunge wa Arusha mjini ambalo mpaka
sasa bado linatumia namba za kawaida na kadi ya gari ikiwa mikononi mwa mbunge
huyo hali inayoonyesha kuwa gari limekabidhiwa kwa halmashauri lakini bado
umiliki wake upo kwa Mbunge huyo.
Diwani wa kata ya
levolosi mh. Efatha Nanyaro, amezungumzia hoja iliyowafanya madiwani kuichangia na kuleta changamoto ni kuhusu uwanja wa mpira wa miguu wa sheikh amri abeid.
Hati iliyopo (nakala) inaonyesha kuwa mmiliki wa uwanja huo ni halmashauri ya jiji na siyo CCM, "kutokana na kuwepo kwa barua kutoka mkoani ilitoa maelekezo kuwa uwanja huo wapewe Chama Cha Mapinduzi ambapo hakuna kikao kilichotoa idhini ya kiwanja hicho kumilikishwa kwa chama cha mapinduzi," alisema Diwani Nanyaro
Hati iliyopo (nakala) inaonyesha kuwa mmiliki wa uwanja huo ni halmashauri ya jiji na siyo CCM, "kutokana na kuwepo kwa barua kutoka mkoani ilitoa maelekezo kuwa uwanja huo wapewe Chama Cha Mapinduzi ambapo hakuna kikao kilichotoa idhini ya kiwanja hicho kumilikishwa kwa chama cha mapinduzi," alisema Diwani Nanyaro
Wakati majibu ya mkurugenzi wa jiji
Athuman Kihamia yakiainisha kuhusu kiwanja hicho kuwa mmiliki wake ni Chama Cha Mapinduzi kutokana na kuwepo kwa kumbukumbu (documents) ofisini kwake hivyo kuwepo kwa kumbukumbu za
nyuma ambazo hazipo katika ofisi ya mkurugenzi hazipo sahihi.
"umiliki wa aridhi unaangaliwa kutokana na mmiliki wa
kwanza amefanya nini katika eneo husika, lakini halmashauri ikiona
mmiliki ameshindwa kuendeleza eneo hilo basi unanyang'anywa na kupewa mtu mwingine
ambaye ana nia ya kuendeleza eneo hilo". amesema Athuman
kihamia.






Post a Comment