Moja ya habari kubwa iliyopo wakati huu ikiwa imejiri
kuanzia usiku wa kuamkia leo ni kuhusu michezo na hususani ya mataifa ya Afrika
iliyokuwa inachezwa mjini Libreville nchini Gabon.
![]() |
| Wachezaji wa Cameroon wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa taji. |
Cameroon wamesherehekea toka usiku wote baada ya klabu
yao kunyakua Kombe la Afrika la Mataifa AFCON usiku wa Jumapilimjini, baada ya
kuilaza Misri mabao mawili kwa moja (2-1)
Ushindi huo unamaliza ukame wa miaka 15 ya Simba wa
Cameroon na kusherehekea ushindi wao wa tano ulipatikana kutokana na mkwaju
ambao haukutajariwa wa Vinncent Aboubacar uliopigwa dakika mbili kabla ya
mchezo kumalizika.
Misri ilifungua mlango wa bao lao la kwanza katika
nusu ya kwanza kutokana na goli lililofungwa na mchezaji wa Arsenal, Mohamed
Elneny, ambaye aliwapatia Wamisri matumaini ya ushindi baada ya kutoshiriki
katika finali hizo tangu 2010.
![]() |
| Wachezaji wa Misri wakishangilia bao lao walilopata wakati wa kipindi cha kwanza. |
Baadaye wachezaji wawili waloingia katika nusu ya kipindi cha pili kwa upande wa Cameroon Nicolas Nkoulou na Aboubakar walibadilisha mchezo ambapo walifanikiwa kuipatia timu yao ushindi waliosubiri kwa muda mrefu.
Ushindi huo pia ulikuwa kwa kocha wao Hugo Broos,
kutoka Ubelgiji aliyekabiliwa na mivutano mikali kutoka kwa vyombo vya habari
tangu kuteuliwa kwake mwezi Februari mwaka jana na kuahidi kubadilisha kabisa
timu hiyo.
"Mimi hufanya
kazi ili kupata matokeo mazuri, na ninafuraha kupindukia kwani tumepata ushindi
wa CAN hii leo. Jambo pekee nililowaambia wachezaji na kuwaomba na kwa sababu
tulifanya kazi nyingi kwa bidi kwa miezi michachache iliyopita ni kua na subira
na kuheshimiana, na nina matumaini vyombo vya habari vitafahamu sasa. Sina
tatizo ikiwa mwandishi wa habari ana mkoso na mchezaji wangu au uwamuzi
ninaoufanya, au chochote kile,lLakini ni lazima iwe kwa heshima." Manasema kocha wa Cameroon Hugo Broos
![]() |
Golikipa wa Cameroon akiokoa moja ya
hatari iliyokuwa langoni kwake.
|
Misri
iliyokua na matumaini makubwa kuweza kulinyakua kombe hilo baada ya miaka 10 ya
kutoshiriki katika finali hizo ililazimika kuwatumia wachezaji wake wawili
wakongwe na wenye ujuzi kwa mafundisho hayo kama Ahmed Fathi na kipa Essam El
Hadary waliocheza kwa pamoja kwa mara saba katika finali ya Kombe hilo la
Afrika.
"Kwanza kabisa nina wapongeza wachezaji
wa Cameroon kwa kunyakua kombe hili, wamecheza vizuri na wanastahili ushindi,
bila shaka ninasikitika na kukasirika lakini kusikitika kwangu ni kwa watu wa
Misri, kwa hakika nilitaka wawe na furaha hii leo kwa kushinda kombe
hili." anasema kocha awa Misri Hector Cuper.



Post a Comment