DAR ES SALAAM.
Wakati mkuu wa Jeshi la
polisi nchini, IGP Ernest Mangu, amewasimamisha kazi askari wapao 12 waliotajwa
kwenye orodha iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya
watu wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya nchini na kudai pia
wao, pamoja na wasanii waliotajwa wanaendelea kuchunguzwa, katika hatua hiyo amedai
kuwa baada ya uchunguzi kukamilika, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaoonekana kuhusika.![]() |
| PHOTO: Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, IGP Ernest Mangu |
Kwa upande mwingine wakati hayo yakijiri, Msanii wa
muziki wa kiazi kipya nchini, Afande Sele ni miongoni mwa wasanii wa siku
nyingi Tanzania ambao wamekua wakifatilia pia na ishu za siasa na mengine
yanayoendelea ambapo leo hii ameandika kuhusu ishu ya dawa za
kulevya iliyotangazwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda.
![]() |
| PHOTO: Selemani Masindi au aka Afande Sele. |
Afande ameandika "Katika hili sakata la MAPAPA
na MAPUNDA ya Unga kama kweli braza Paul yupo serious na sio ‘Matango Pori’ kama
tulivyoona ktk masakata mengine,huenda hata wale WASAFI wakaonekana
wachafu…kila la kheri Mr Paul….RiP Da Amina…wacha parry ianzeee"
Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram aliposti kama ifuatavyo:....
![]() |
| PHOTO: Kutoka ukurasa instagram wa Selemani Masindi -Afande Sele |
this story firstly it was appeared from some blogs



Post a Comment