Baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam kutangaza majina ya wahusika wanaojiushisha na madawa ya kulevya skendo hiyo inaendelea baaada ya watuhumiwa 13 wa matumizi ya dawa hizo za kulevya wakiwemo wasanii maarufu watakuwa chini ya uangalizi wa jeshi la polisi pamoja na mahakama.
![]() |
| PHOTO: Baadhi ya watuhumiwa wa kesi ya madawa ya kulevya wakiwa mahakamani jijini Dar Es Salaam. |
![]() |
PHOTO: Watuhumiwa wa kesi ya madawa ya kulevya wakiingizwa
mahakamani.
|
DAR ES SALAAM.
Watuhumiwa waliofikishwa kwenye mahakama ya Kisutu hapo
jana, akiwemo msanii Wema Sepetu ambaye
shauri linalomhusu bado shauli lake bado hatma yake haijajulikani itakuwa lini,
ikiwa bado anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es
salaam.
Watuhumiwa waliopandishwa kizimbani mpaka jana ni pamoja
na Khaleed Mohamed (TID), Hamid Salum Chambuso, Rachel, Tunda Kimaro, na Joan,
pamoja na hao kuna watu wengine maarufu kadhaa nao inasemekana wanaendelea
kuhojiwa juu ya tuhuma hizo za kujihusisha na dawa za kulevya.
Kupitia hati ya kiapo cha iliyotolewa mahakamani hapo,
mahakama imetoa masharti ya watuhumiwa hao kuwa chini ya uangalizi wa jeshi la
polisi na mahakama kati ya mwaka moja hadi mitatu kwa ajili ya kuangalia
mienendo yao.
Upande
wa mahakama chini ya kiapo cha mkuu wa kitengo cha polisi cha kupambana na dawa za
kulevya ASP Denis Mnyumba umeiomba mahakama kutoa kiapo kwa watuhumiwa ikiwemo
uangalizi wa kipindi kisichozidi miaka 3 huku wahusika wakitakiwa kuripoti
polisi mara mbili kwa mwezi,ili kufuatilia mwenendo wa tabia zao.



Post a Comment