0
Viongozi wa Afrika waliokutana mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, waliunga mkono mpango wa Kenya wa kujiondoa kwa pamoja katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
ADDIS ABABA
Viongozi wa Umoja wa Afrka AU wakiwa katika picha ya pamoja.

Viongozi wengi wa umoja huo wanahisi kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inawalenga viongozi wa bara la Afrika pekee, viongozi hao wanasema kuwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ilifanya makosa kwa kumlenga rais wa Sudan Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.
Rais wa Chad Idriss Deby alisema;"Tathimini yetu ni kwamba ICC inalenga zaidi mataifa ya Afrika, hasa viongozi wa nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na viongozi walio madarakani, wakati ambapo kwingineko duniani, mambo mengi yanayotokea, ukiukwaji mkubwa ulio wazi wa haki za binadamu, lakini hakuna kiongozi anayefuatiliwa, watu wote ni sawa mbele ya sheria, na sheria iko juu kwa kila mtu."
Jumamosi baada ya kuchaguliwa kwa rais mpya wa Umoja wa Afrika. "Kwa hiyo tumeamua kutoa msimamo wetu kwa kusubiri Mahakama ya ICC ichukuwe hatua muhimu kwa msimamo wa viongozi wa Afrika kuhusu suala hili," Bw Deby aliongeza.
Lakini serikali ya Kenya ambayo kwa muda mrefu imekua ikikosoa Mahakam ya ICC ilitoa pendekezo kwa Umoja wa Afrika ili kuendeleza mkakati kwa wa nchi za Afrika kujiondoa katika Mahakam ya ICC, pendekezo ambalo lilipitishwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika.

Post a Comment

 
Top