0
Mtoto mchanga aliyeibwa miaka 18 iliyopita katika hospitali moja iliyopo kwenye jimbo la Florida nchini Marekani, amepatikana akiwa hai katika jimbo lingine la South Carolina.

Mtoto aliyeibwa Kamiyah Mobley kushoto na mwanamke aliyepatikana naye Gloria Williams Kulia

MAREKANI:
Mtoto huyo Kamiyah Mobley, aliibwa kutoka kwa mama yake akiwa na umri wa saa 8 pekee toka kuzaliwa.

Mwanamke mmoja ambaye alijifanya kuwa ni  muuguzi katika hospiali hiyo alisema mtoto huyo alikuwa mgonjwa hivyo anahitaji uchunguzi wa kina wa kimatibabu.

Hata hivyo baadaye alitoweka na mtoto huyo, ambapo mwanamke anayeishi na mtoto huyo, Gloria Williams, alitiwa mbaroni baada ya polisi kupewa ripoti kuhusu mtoto.

Familia halisi ya mtoto huyo ilipewa taarifa kuhusu kupatikana kwake baada ya uchunguzi wa vinasaba kubaini utambulisho wake.

Post a Comment

 
Top