0

DAR ES SALAAM,
Mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana katika nchi za Afrika kama AFCON yamefunguliwa rasmi nchini GABON huku kampuni ya Multchoice yenye makao makuu yake nchini Afrika Kusini na kuwa na ofisi katika nchi kadhaa dunia na ambayo ndiyo inayorusha matangazo hayo moja kwa moja, imefanya uzinduzi huo moja kwa moja kutoka nchini Gabon.

Wakati msanii wa kizazi kipya nchini Diamond akipata nafasi ya kuimba katika ufunguzi huo, hapa nchini uzinduzi huo umefanyika jijini Dar Es Salaam katika bustani ya Shekinal iliyopo Mbezi Beach na kuhudhuliwa na wafanyakazi wa Multchoice Tanzania pamoja na wanahabari kadhaa waliokuwepo,


Hapa chini tunakuletea picha chache ambazo camera ya TODAYS NEWS ilifanikiwa kunasa matukio kadhaa tuliyopata…

Kikundi cha muziki wa nyimbo ambacho kilikuwa kikiburudisha watu katika shughuli nzima jijini Dar Es Salaam.
Wafanyakazi wa Multchoice Tanzania wakiwa na Mkurugenzi wao mwenye t-shirt nyeusi Salum Salum anayeongea wakati wa tafrija fupi ya ufunguzi wa mashindano ya Mataifa ya Afrika - AFCON
Wafanyakazi DStv na Wanahabari wakiburudika kabla ya ufunguzi rasmi wa maonyesho ya mpira wa miguu kwa mataifa ya Africa kupitia DStv
Wakati wa kushuhudia ufunguzi wa mashindano hayo kupitia Screen kubwa iliyokuwepo hapo yanayorushwa na DStv hakuna aliyekubali kukaa chini na kuacha kila kitu mezani, moja ni kumshuhudia kijana wa Kitanzania aliyepata nafasi kuimba katika ufunguzi huo, Diamond Platnumz.


Hapa tulifanikiwa kupata moja ya clip-photo kupitia Screen ambayo Diamond alipokuwa akiimba pamoja na wacheza wake katika ufunguzi huo wa michezo hiyo huko nchini GABON.





Post a Comment

 
Top