Mkate ulikwenye mashine ya kutengeneza toast ukiwa tayari umebadirika rangi kwa kuliwa. |
AFYA.
Mkate, Chipsi na Viazi pamoja na vyakula vingine havifai kuchomwa au kupikwa hadi kupata rangi ya hudhurungi, wataalamu wameonya, badala yake wanasema zinafaa kupikwa hadi viwe na rangi ya manjano iliyokolea ikiwa na rangi ya dhahabu.
Wanasema hilo litapunguza ulaji wa kemikali ambayo huenda inachangia saratani aina ya Acrylamide ambayo huzalishwa wakati vyakula vyenye wanga vinapochomwa au kukaangwa kwa muda mrefu katika kiwango cha juu sana cha joto.
Wakala wa viwango vya ubora vya chakula nchini Uingereza (FSA) anapendekeza wapishi wafuate vema maagizo ya mapishi wakati wa kupika na wasiache chakula kipate rangi ya kahawia.
Shirika moja la kukabiliana na kansa la Cancer Research UK, limetoa taarifa na kusema kuwa, hata hivyo uhusiano wa moja kwa moja kati ya Acrylamide na saratani miongoni mwa binadamu haujathibitishwa.
Wakala wa viwango vya ubora wa chakula anasema kwamba viazi na mboga aina ya karoti ziitwazo parsnips hazifai kuhifadhiwa kwenye friji, hii ni kwa sababu viwango vya sukari kwenye mboga huongezeka zinapohifadhiwa kwenye viwango vya chini sana vya joto (mazingira baridi) na hivyo kuongeza kiasi cha Acrylamide inayozalishwa chakula kinapopikwa.
Acrylamide hupatikana katika vyakula vingi na huzalishwa chakula kinapopikwa, viwango vya juu vya kemikali hiyo hupatikana wakati wa mapishi, vyakula vyenye viwango vya juu vya wanga kama vile viazi, vibanzi (chipsi), mkate na parsnips, vinapookwa, kuchomwa au kukaangwa katika viwango vya juu sana vya joto.
Viwango vya juu vya acrylamide hupatikana kwenye vyakula vyenye kiwango cha juu cha wanga vinapopikwa viwandani kwa joto ya zaidi ya nyuzi joto 120C, kama vile kaukau, mkate, biskuti, keki na kahawa.
Aidha, huzalishwa nyumbani wakati wa kupika vyakula vyenye viwango vya juu vya wanga kama vile viazi, chipsi, mkate na pasnips kwa kuoka, kuchoma au kukaanga katika kiwango cha juu sana cha joto, mkate unapochomwa na kutengeneza tosti, kwa mfano huzalisha acrylamide zaidi.
Wakati wa chakula kubadilika rangi na kuwa cha hudhurungi, sukari, amino asidi na maji kwenye mkate hushikana na kutengeneza rangi na acrylamide - pamoja na ladha tamu na harufu nzuri.
Source BBC
Post a Comment