Taasisi ya elimu
Tanzania ni taasisi ya serikali iliyochini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ikiwa na majukumu kuweza kuboresha mitaala ya elimumsingi ambayo ni
mtaala wa elimu ya Awali, Mtaala wa darasa la I – VI, ikiwemo mtaala wa
sekondari na wa Walimu. Kuandaa vifaa vya kufundishia na kujifunza, miongozo ya
walimu, kutoa mafunzo juu ya mitaala iliyoboreshwa na kufanya utafiti kujua
mahitaji halisi ya jamii na dunia kwa ujumla.
Mwalimu Esta Molelidina Laiza kutoka OlijoroL Arusha akigani beti za wimbo wa ngonjera katika sherehe za kufunga mafunzo
wengine ni walimu wenzake waliokuwa wakiunga mkono kiitikio.
|
Walimu waliohudhulia mafunzo ya walimu wa elimu ya awali waliyofanyika katika chuo cha ualimu Patandi Arusha wakifuatilia ngonjera. |
Meza kuu wakiongozwa na Mthibiti mkuu
wa ubora wa elimu kanda ya kaskazini magharibi (mwenye kipara) wakifuatilia
matukio huku wakisoma taarifa mbalimbali za mafunzo hayo.
|
Mwalimu Edina Laiza kutoka OLKIU wilaya
Ngorongoro akigani beti za wimbo wa ngonjera katika sherehe za kufunga mafunzo
wengine ni walimu wenzake waliokuwa wakiunga mkono kiitikio.
|
Walimu waliohudhulia mafunzo ya walimu wa elimu ya awali waliyofanyika katika chuo cha ualimu Patandi Arusha wakifuatilia ngonjera. |
Mwalimu Elibariki Kaaya kutoka
simanjiro akisoma risala kwa niaba ya walimu wenzake kwa mgeni rasmi (hayupo
pichani)
|
Walimu waliohudhulia mafunzo ya walimu wa elimu ya awali waliyofanyika katika chuo cha ualimu Patandi Arusha wakifuatilia hotuba ya Mwl Elineema. (hayupo pichani) |
Mmoja wa walimu Alais Lailorye (mwenye
koti jeusi) wa jamii ya kimasai anayefundisha kwa kujitolea huku akiwa na umri mkubwa
akikadilia miaka zaidi ya 60.
|
Zena Rashid ambaye ni Mkuza mitaala
Taasisi ya Elimu Tanzania akitoa hotuba ya shukurani wakati wa kufunga mafunzo
ya walimu wa elimu ya awali jijini Arusha.
|
Victor Bwindiki –Zonal Chief School
Quality Assurance Officer, akitoa hotuba ya kuhairisha mafunzo ya walimu kutoka
katika kanda yake jijini Arusha.
|
ARUSHA.
Katika
hotuba yao ya kufunga mafunzo hayo ya walimu wa elimu ya awali yaliyofanyika
jijini Arusha katika chuo cha walimu Patandi, wameuomba uongozi wa Taasisi ya
Elimu kuongeza nafasi ya mafunzo kwa walimu wa elimu ya awali pamoja na kwamba
wanashukuru kwa nafasi iliyopatikana kujifunza mbini mbalimbali
zitakazowasaidia kufikia malengo pamoja na kuboresha elimu kwa ujumla.
katika hotuba yake kwa
mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuza mitaala kutoka Taasisi ya
Elimu (TET) Zena Hashim Amir amesema kuwa; lengo kuu la mafunzo hayo lilikuwa
kuwajengea walimu wa elimu ya awali uwezo
wa kutekeleza mtaala na muhtasari wa elimu ya awali ulioboreshwa wa mwaka 2016.
“tunatarajia baada ya mafunzo haya kila mshiriki ataweza; kukuza
uelewa wa dhana mtaala, kutumia mtaala na vifaa vyake, kubaini, kufaragua,
kutengeneza na kutumia zana stahiki katika kufundishia na kujifunzia, kujenga
uwezo wa kufanya maandalizi ya ufundishaji pamoja na kumwezesha mwalimu kujenga
uwezo wa kuhusisha kitabu na umahiri husika” alisema
Zena Hashim.
Mafunzo hayo
yaliyokusanya walimu kutoka mikoa miwili ya Arusha na Manyara, yalionyesha
kufanikiwa mara baaada ya mmoja wa walimu aliyekuwepo katika mafunzo hayo
ambaye anatoka katika jamii ya kimasai Alais Lailorye ambaye alifanya
vizuri katika mitihani na kutokana na kutokuwa na elimu kubwa ya ufundishaji
kama walivyo walimu wengine, yeye hakusoma sana lakini ameweza kuwa mwalimu na
kujivumia kutoa watoto wanaojua kusoma na kuandika katika eneo analotoka.
”mimi nimejitolea kufanya kazi hii baada ya kuona watoto wetu wa
jamii ya kimasai wanakosa elimu na nilianza kwa kutumia vitabu nilivyoachiwa, hivyo
nikaamua kuanzisha darasa la awali kuweza kuwafundisha sarufi na silipwi na mtu
yeyote watoto ninaowafundisha huko kijijini kwetu na wanafurahia sana kusoma,
japo natamani na mimi niweze kulipwa kama wengine”
anasema Alais Lailorye mwenye miaka 60 anakadilia.
Mthibiti mkuu ubora wa
shule kanda ya Kaskazini Magharibi, Arusha na Manyara Victor Bwindiki amefunga
mafunzo hayo huku akiwahasa walimu waliohudhulia mafunzo hayo kuwa, serikali ya
awamu ya tano inalenga katika kuleta mbadariko makubwa ya kiuchumi nakufikia uchumi
wa kati kama nchi nyingine, huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Magufuri akitaka mabadiriko kupitia elimu.
Anasema Bwindiki “Hivyo hakuna
mtu mwingine atakayeleta mabadiriko katika elimu zaidi ya walimu mnaofundisha
watoto wa elimu ya awali, mnayo nafasi muhimu kuwaandaa na kuwajengea watoto
stadi za msingi za kujifunza, kupitia taaluma stahiki mtakayowezeshwa, pia ni
wajibu wenu mkubwa huko muendako mkalete mabadiriko katika sekta ya elimukwa
kuwaelekeza wenzenu ambao hawakupata fursa ya kuhudhulia mafunzo haya.”
Pia kupitia muongozo wa
ufundishaji wa elimu ya awali michezo ina nafasi kubwa katika kuwajengea watoto
uwezo na kuwapa hamasa ya kupenda kuhudhulia shule.
Post a Comment