Bw
Barrow alipokelewa nchini Senegal tangu Januari 15 kufuatia ombi la Jumuiya ya
Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo ilikua ikihofia
usalama wake endapo BwJammeh atakua bado madarakani.
Rais
wa Gambia Adam Barrow ambaye jioni hii amerejea nyumbani akiongozana na mjumbe
maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Afrika Magharibi.
|
GAMBIA/ECOWAS
Rais wa Gambia Adama Barrow ametazamiwa
kurejea leo nchini Gambia, huku wananchi wengi wakiwa wanamsubiri toka alipoapishwa
wiki moja iliyopita katika ubalozi wa mdogo mjini Dakar nchini Senegal baada ya
kuondoka kwa Yahya Jammeh Januari 21, rais huyo mteule alikua amepinga kurejea
nchini kwake wakati ambapo alikuwa akihofia usalam wake.
Gambia ni taifa dogo linalozungumza Kiingereza huku likizungukwa
na Senegal, isipokuwa eneo dogo la pwani ambako watalii wengi hutembelea, liliongozwa
kwa mkono wa chuma kwa miaka 22 na Yahya Jammeh, ambaye ni mwanajeshi wa
zamani.
Rais Adama Barrow ametangaza kurejea nchini Gambia Alhamisi
hii majira ya saa 10:00 kwa saa za kimataifa (International Greenwich) kupitia
ukurasa wake wa facebook, hata hivyo kurejea kwake nchini Gambia kumethibitishwa
na chanzo cha Ofisi ya rais wa Senegal na baadaye washirika wa karibu wa rais
wa Senegal na Gambia.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Afrika Magharibi,
Mohamed Ibn Chambas, ambaye alilialifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kuhusu hali hiyo katika kikao cha faragha, ataongozana na Barrow kutoka Dakar
kwenda Banjul, kwa mujibu wa chanzo cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Source RFI
Post a Comment