0
Imeelezwa kuwa teknolojia duni,rasilimali fedha,malighafi kuwa juu, uhaba wa mvua unaotokana na uharibifu wa mazingira ndio changamoto kubwa inayomkabili mkulima wa Tanzania kutofikia malengo ya kufanya kilimo biashara.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamba wakati wa kufungua maonyesho ya kilimo –Selian Arusha.
ARUSHA.
Hayo yamebainishwa na mkuu na mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Daqarro kwenye Maonyesho ya zana za kilimo yanayojulikana AGRItech EXPRO TANZANIA yamefunguliwa jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika jijini hapo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani iliyopo mkoani hapa na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.


Wageni rasmi waliofika wakati wa ufunguzi wa maonyesho yanayojulikana kwa jina AGRItech EXPRO 2017 TANZANIA, kutoka kulia ni Daniel Loiruck –Afisa kilimo wa mkoa Arusha, Eric Ng’amaryo –Mwenyekiti TAHA Taifa, Fabian Daqarro –Mkuu wa wilaya ya Arusha, Dr, January Mafuru –Mkurugenzi utafiti wa kilimo kanda ya kasikazini (Sari)  

Mshauri wa mambo ya uchumi kutoka wizara ya kilimo na chakula Profesa Aden Nyange akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kilimo AGRItech.

Baadhi ya wadau wa kilimo na wataalam ambao wamehudhulia ufunguzi wakisikiliza kwa makini mkuu wa wilaya alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi.
Alan Edwards meneja masoko kanda ya Afrika akitoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian alipotembelea banda lao mapema leo.



Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni tanzu ya kilimo PASS huku meneja usimamizi maarifa na mawasiliano wa AMDT Al-amani Mutarubukwa akisikiliza akiwa kashika kifaa kimoja kinachohusika katika kilimo.

Meneja wa masoko wa kampuni ya GSI Group ya Afrika kusini akimpa maelezo mkuu wa wilaya ya Arusha jinsi kampuni yao inavyozalisha vyakula vyenye uwezo wa kumfanya kuku kufikia uzito wa kilo 5!
Mashine saidizi ya kubebea mizigo ambayo imetengenezwa na kampani ya BUV Tanzania, Scott Price aliyekaa juu ya pikipiki hiyo anamuonyesha mkuu wa wilaya (kulia) jinsi inavyofanya kazi.
Mkuu wa wilaya ya Arusha pia alipata nafasi kutembelea banda linaloonyesha uzalishaji wa nyanya, hapa Butwa Godluck meneja masoko na mauzo akitoa maelezo.




HABARI KWA UNDANI..
Hayo yamebainishwa na mkuu na mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Daqarro kwenye Maonyesho ya zana za kilimo yanayojulikana AGRItech EXPRO TANZANIA yamefunguliwa jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika jijini hapo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani iliyopo mkoani hapa na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Vilevile amesema kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa 
wa Arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa siku mbili, hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kujifunza teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wa wataalamu mbalimbali, ukaowasidia kuendesha kilimo chenye tija.
“serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaangalia ni kwa namna gani wataweza kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini”, Amesema Fabian Daqarro.

Amewataka wadau hao wa maonyesho hayo ya kilimo kuangalia namna bei za pembejeo za kilimo, kwani inaonyesha asilimia kati ya 75-80 ni ya wakulima wadogo wadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili mkulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua pembejeo hizo ili waweze kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo, katika uzalishaji wa Teknolojia ,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.
“Sisi Seliani tupo tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi taongezeka pamoja na wakulima watafahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wa mazao” amesema Dr. Mafuru.

Post a Comment

 
Top