Wananchi wengi wenye magari ambao mara nyingi
wanakuwa wakibuni kila siku kuyafanyia marekebisho au kuyapamba ili kuweza
kubadirisha muonekano au hata kuongeza baadhi ya vitu zikiwepo taa za aina
mbalimbali wamekuwa wakifanya hivyo kwa lengo ambalo kila mmoja ana madhumini
yake.
Kamanda wa Polisi kikosi cha usalama
barabarani nchi Mohamed Mpinga akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu
sheria mpya wa wenye magari yenye kutumia spotlight wakati wote.
|
DAR ES SALAAM
Jeshi
la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabarani kwa matumizi kusudiwa ya
taa kadiri ya mfumo wake yanayohusiana na usalama barabarani sura ya 168 ya
mwaka 2002 na kwa kutambua umuhimu wake katika kifungu cha 38(1) na 39 C
imepiga marufuku matumizi ya taa zenye kuongeza mwanga wa ziada, ikimaanisha
kuwa taa zikitumika vibaya ni chanzo cha ajali.
Akiongea na
wanahabari jijini Dar Es Salaam kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini
DCP Mohamed Mpinga amesema katika gari kuna zipo taa za aina mbili ambazo kazi
yake ni kumulika mbele, vilevile zipo taa zitumikaz0 kumulika pembeni (indiketa),
zipo taa za kutoa ishara ya breki, taa za maegesho , taa za kuashiria kurudi
nyuma na taa za ndani ikiwa ni pamoja na za kwenye dashboard.
Kamanda DCP Mpinga aliyenyoonya mkono
akiongea na wanahabari huku maafisa wa polisi kutoka kikosi cha usalama
barabarani wakimsikiliza.
|
“yapo magari hususani makubwa ya mizigo na hata ya abilia ambayo
yamefanya marekebisho kwa kuongeza taa (spot light) ambazo hazikuwekwa na
mtengenezaji na huzitumia taa hizo na kuhatarisha usalama barabarani, taa hizi
hutumika vibaya hasa nyakati za usiku na kuwa chanzo cha ajali kwa kuwa
zinapotumika hupoteza uwezo wa mtumiaji mwingine wa barabara kuweza kuona mbele”
Alisema kamanda Mpinga.
Hata hivyo katika
kubainisha ajali ngapi zimetokea kutokana na matumizi mabaya ya taa kwa mwaka
2015 ni 104 na mwaka 2016 ni ajali 123 na mpaka sasa idadi ya magari
yaliyotolewa taa hizo ni 665 toka zoezi hilo lianze na mkoa ambao umekuwa
ukipata malalamiko kutokana na kutotenda haki kwa wasafirishaji wengine
kutoondolewa taa hizo kwenye magari yao.
Habari zaidi ili uweze
kusikiliza kwa undani alichosema nitakuletea katika T NEWS.
Post a Comment