0
Mkurugenzi wa Elimu na huduma kwa mlipa kodi Richard Kayombo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mapema leo ambapo mamlaka hiyo imefikia.


Mkurugenzi wa Elimu na huduma kwa mlipa kodi Richard Kayombo kulia akiwasilisha mlinganisho wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2015/2016 kwa wanahabari.

DAR ES SALAAM.

Mamlaka ya mapato nchini yatoa taarifa kutokana na makusanya ya mapato kwa kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2016/2017 kuanzia julai hadi desemba 2016, ambapo mamlaka hiyo imekusanya kodi jumla ya shilingi 7.27 trilioni ikilinganishwa na shilingi 6.44 trilioni ambazo zilikusanywa kwa kipindi hicho cha mwaka wa fedha 2015/2016.

Hata hivyo katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatilia, kuhimiza matumizi ya mashine za kieletroniki na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.

Mkurugenzi wa elimu na huduma kwa mlipa kodi Richard Kayombo anasema "tunawakumbusha wananchi wa Dar Es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za namba ya Utambulisha wa mlipa kodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31Januari2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa kwa mikoa mingine".

.

Post a Comment

 
Top