Kufuatia kuenenea kwa wafanyabiashara wa kila aina mitaani
wakiwemo wale wanaouza biadhaa za mapanga na visu ambao mara kadhaa wamekuwa
wakionekana katika njia panda pananakuwepo na taa za kuongozea magari (Traffic
Light).
Kamishina wa polisi wa kanda hiyo Simon Sirro. |
DAR ES SALAAM.
Jeshi la polisi kanda maalum jijini Dar es
salaam limepiga marufuku wafanyabiashara wanaouza visu, mishale, majambia
pamoja na mapanga hadharani pasipokuwa na kibali cha jeshi hilo .
Akizungumza na
waandishi wa habari Kamishina wa polisi wa kanda hiyo Simon Sirro amesema hatua
hiyo yakupiga marufuku uzwaji wabidhaa hizo imetokana baadhi ya watu wasio
waaminifu kutumia silaha hizo kufanya uhalifu ikiwemo unyang'anyi.
'' kuanzia leo hatutaki biashara ya visu, mishale pamoja
mapanga barabarani ukitaka kuuza bidhaa hizi lazima uwe naleseni maalum''Alisema Kamishina Simon Sirro. Hata hivyo
ameongeza kuwa, sambamba na kupiga marufuku uuzwaji wa mishale pamoja na mapanga
pia ameweza kupiga marufuku uuzwaji wa manati barabarani.
Katika hatua
nyingine jeshi hilo linatarajia kuadhimisha siku ya polisi kuanzia kesho ambapo
maadhimiasho hayo yanatarajiwa kuhudhuliwa na waziri wa mambo ya ndani Mwigulu
Lameck Nchemba.
Post a Comment