0
Kufuatia sekeseke la kauli tata za Rais wa Marekani zisizopendwa na baadhi ya raia wa marekani na wengine kutoka mataifa kadhaa ya nje ya marekani, hasa baada ya kusaini sheria ya kuzuia waislamu kuingia nchini humo, kauli hizo zimepelekea hali ya sintofahamu kutokana na upepo kubadirika kila uchao nchini humo.


Profile: Waandamanaji nchini Marekani wakiwa na mabango yanayomkataa Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates masaama chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.

Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu mwanasheria huyo kwa usaliti, Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kuwa marufuku hiyo iliyowekwa ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.


Mwanasheria mkuu aliyeachishwa kazi kutokana kutokukubaliana na matamko na sheria anazotoa Trump pia amekuwa akiwaunga mkono waandamanaji.
Baada ya kuondolewa katika wadhifa wake nafasi yake imechukuliwa na kiongozi wa mashtaka kutoka mahakama ya kijimbo ya huko Virginia Dana Boente.
Agizo hilo la Rais Trump lililotiwa saini Ijumaa iliyopita limesababisha maandamano nchini Marekani pamoja na nchi za ughaibuni, ambapo hapo awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.


Source BBC

Post a Comment

 
Top