![]() |
| Mtendaji mkuu (CEO) wa RECSA Theoneste Mutsindashyaka akitoa hotuba wakati wa kufungua mafunzo hayo kwa askari wa jeshi la polisi nchini |
![]() |
| Maofisa wa jeshi la polisi kutoka mikoa kadhaa nchini wakimsikiliza Meneja wa kanda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanayofanyika jijini Arusha |
![]() |
Dennis
F. Hadrick ni meneja mipango kutoka Marekani chini ya ofisi inayohusika na
mambo ya siasa na kuondoa silaha ndogondogo katika nchi kadhaa kwa ukanda wa Afrika mashariki na maziwa makuu.
|
![]() |
Maofisa
wa jeshi la polisi kutoka mikoa kadhaa nchini wakiwa tayari kwa mafunzo
yanafanyika katika hotel ya Veta Njiro jijini Arusha.
|
![]() |
Naibu
kamishna wa polisi Charles Mkumbo akifungua mafunzo ya yenye lengo la
kuwawezesha askari kuwa na uwezo wa kuthibiti siraha ndogondogo na zisizo rasmi
kwa raia.
|
![]() |
| Heshima kwa nyimbo za Taifa ikifanyika wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa Taifa wa Tanzania na Marekani kabla ya kuanza mafunzo hayo. |
![]() |
Kamandi
ya mafunzo ikiwa katika hali ya saruti kuonyesha heshima kwa nyimbo za Taifa za
Marekani na Tanzania.
|
![]() |
Kamandi
ya mafunzo kutoka nchi tatu; kutoka kushoto ni Maj. P.Kairuki -Kenya, Lt Frank
Kamanzi -Rwanda, Capt. Justin Pamba –Kenya, Lt. Silver Maari –Uganda na Capt.
Steven Banyaga –Rwanda.
|
ARUSHA.
Ueneaji
wa silaha zisizo salama miongoni mwa jamii zilizo katika ukanda wa Afrika
mashariki, kusini mwa jangwa la sahara // nchi jumuiya ya SADC limekuwa ni
janga linalosababisha matukio ya uharifu na uvunjifu wa Amani katika nchi hizo,
ambapo kufuatia hali hiyo kituo cha kikanda cha uthibiti wa silaha ndogondogo Reginal
Centre on Small Arms (RECSA) inayondesha mafunzo katika nchi hizo ili
kuhakikisha tatizo la umiliki wa silaha holela unapungua kama si kuisha kabisa.
Ikiwa jeshi la polisi
ndilo moja ya jeshi hapa nchini lenye mamlaka ya kutunza na kuthibiti silaha, mafunzo kwa
askari kutoka vikosi vya jeshi la polisi nchini yanatolewa ikiwa ni njia
mojawapo itakayowasaidia kutambua siraha hatarishi na kuthibiti silaha hizo.
Akifungua mafunzo hayo
mkoani Arusha, Naibu kamishna wa polisi Charles Mkumbo amesema mafunzo hayo
yatawawezesha askari wa jeshi hilo kuwa na utaalam utakaowawezesha kutunza
silaha ndogodogo ambapo utaalam watakaofundishwa na kuelewa umuhimu wa kutunza silaha
ikiwa ni pamoja na kuziwekea alama silaha zote ndogondogo ikiwa ni pamoja na
silaha zilizopo uraiani, ambapo hapo nyuma kumekuwa na zoezi kama hilo la
kutambua siraha zote zilizo mikononi mwa raia.
Ni kweli kwamba kama usimamizi wa uhifadhi utaboreshwa basi idadi halisi ya silaha itakayopatikana itakuwa inajulikana, hii itatoa nafasi itayosaidia kutoa utambulisho wa zilizopo na zilizopotea” anasema kamishina Mkumbo.
Mpango huu unaoratibiwa na RECSA ambao kwa mara ya kwanza ulianza mwaka 2004, ukihasisiwa na nchi zilizo katika pembe ya Afrika na zile za maziwa makuu, ulifahamika kama Itifaki ya Nairobi kwa ajili ya kuzuia, kuthibiti na kupunguza ueneaji wa silaha ndogondogo na nyepesi.
Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na moja kwa moja na serikali ya marekani kwa ushirikiano kati ya Mpango wa kanda wa kuzuia silaha ndogondogo -RECSA na WRA unajumuisha nchi zaidi ya 6 ambazo zote kwa pamoja zimetoa wakufunzi wanaozungukan katika nchi tofauti kwa lengo la kutoa elimu wa majeshi husika.

Post a Comment