0
Rehema Chalamila enzi zake wakati akiwa kwenye chati ya muziki
wa kizazi kipya ‘aka’ Bongo fleva.

DAR ES SALAAM
Wakati idadi ya wasanii wanaotumia dawa za kulevya nchini ikiendelea kuongezeka huku vijana wengi na hata ukanda wa Afrika mashariki wakiona ndiyo suluhu ya kumaliza matatizo yao, Serikali imeanzisha msako dhidi ya wauzaji na waingizaji wa dawa za kulevya nchini humo.

Hatua hii ya Serikali imekuja baada ya hivi karibuni kuonekana wimbi la wasanii wanaotumia dawa za kulevya likiendelea kuongezeka na kutishia mustakabali wa vijana ambao wamo kwenye tasnia hiyo.
Ray C akiwa jukwaani kutumbuiza mashabiki enzi za kiumo hakina mfupa.
Hivi karibuni mmoja wa wasanii waliowahi kuvuma sana kwenye muziki Chid Benzi ambaye hali yake imeendelea kuzorota kutokana na kuathirika kwa kiasi kubwa na dawa za kulevya, alimaarufu kwa kipindi cha nyuma “unga” na sasa unafahamika kama “sembe”.
Msanii huyu licha ya kuwahi kupelekwa katika kituo maalumu kinachotoa huduma kwa watu walioathirika na dawa za kulevya, mara baada ya kutoka bado hali yake si nzuri, alirejea tena katika kutumia unga, hali inayomfanya sasa kukosa usaidizi wa aina yoyote ili kuweza kumnusuru.
Huyu ni mwanamuziki Chidi Benz kushoto akiwa bado hajapata madahara enzi zake na kulia akiwa katika hali mbaya kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Mbali na Chid Benz, yuko pia msanii wa kike aliyewahi kuvuma hapa nchini na Afrika mashariki jina maarufu kama “Ray C” Rehema Chalamila, yeye aliwahi kupokea msaada kutoka kwa aliyekuwa rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete ambaye alilipia gharama za matibabu yake, lakini nae baada ya kutoka huko alirejea kutumia unga.
Mbali na wasanii hawa, wamo pia wasaani wengine wengi wanaoimba, kuigiza na sanaa nyingine ambao nao wanajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo bila kujua wanajikuta wanashindwa kuacha na kuathirika pakubwa.
Baadhi ya wananchi wameonesha kuchukizwa na ongezeko la vijana maarufu kujitumbukiza kwenye matumizi ya dawa hizo, ambazo wanasema kamwe haziwezi kumaliza matatizo yao bali zaidi ni kuongeza mzigo kwa jamii na familia zao.

Baada ya kupata taarifa mbalimbali pia kutoka jeshi la poilisi, habari hii inaendelea kwenye kurasa ya tarehe 13.01.2017 >>>>

Post a Comment

 
Top