0
Rais Dr. John Pombe Magufuri.
DAR ES SALAAM.
Wafanyabiashara wa viumbe hai wa polini wamemuomba Rais John Mugufuli asikie kilio chao na kufungulia biashara yao ya kusafirisha viumbe hao nje ya nchi baada ya serikali kupiga marufuku usafirishaji huo tangu mwanzoni mwa mwaka huu

Wafanyabiashara hao walivamia Wizara ya Maliasili na Utalii na kuonana na Waziri mwenye dhamana Prof.Jumanne Maghembe kuhusu kilio chao hicho cha kutaka serikali ifungulie biashara hiyo ya uuzaji wa viumbe pori hai nje ya nchi.
Akizungumza kuhusu sakata hilo, Prof. Maghembe amesema kimsingi Serikali imepiga marufuku biashara ya kusafirisha kuanzia Machi 17 mwaka huu, Serikali ilisimamisha ghafla usafirishaji wa viumbe pori hai nje ya nchi, hatua iliyokuja baada ya wafanyabiashara hao kulipia gharama zote wizarani ikiwemo vibali, hivyo wametaka rais kuingilia kati jambo hilo.
Mjusikafiri anakimbia kwa wepesi wa aina yake.
“serikali imekataza kwa angalau miaka mitatu biashara hii iachwe ili idara ya wanyamapori ijipange namna ya kufanya biashara hii kwa usalama, uhakika na kwa kufuata sheria na sababu kubwa za serikali kuchukua hatua hiyo ni kwanza wanyama wa Tanzania wanakamatwa katika bandari na viwanja vya ndege vya nje ya nchi wakiwa hawakufuata taratibu za kusafirishwa.”amesema waziri Prof. Maghembe.
Pamoja na hayo Mh. Maghembe amesema wataalamu wa wizara wanaendelea na uhakiki wa vibali vya wafanyabiashara hao ili wajue namna ya kuwalipa kifuta jasho.

Post a Comment

 
Top