0
Moto ulioteketeza jengo hilo lililokuwa limezeeka
Watu zaidi ya watu 30 wamefariki kutokana na moto ulioteketeza ghara moja na mpaka kufikia jana Jumapili waliongezeka na kufikia 33.


Inasemekana na huenda ikaongozeka mpaka kufikia watu 40, wakati waokoaji wakiendelea kutafuta miili zaidi kwenye mabaki ya jengo lililoungua ambapo densi iliyopambwa kieletroniki ambapo ilishika moto.

Mara baada ya kuzimwa.
Moto huo uliotokea katika mji Oakland California nchini Marekani siku ya Jumapili usiku unasemekana ni asilimia 20 tu pekee ya jengo hilo ndiyo iliyokuwa imefikiwa.
Melinda Dayton ambaye ni afisa kutoka idara ya zimamoto  alisema kuwa shughuli ya uokoaji haikuwa rahisi lakini akaongeza kuwa heshima ya waathirika pamoja na familia zao ingetiliwa mkazo na kuendelewa kutunzwa.
Maafisa wanaendelea kuchunguza ili kubaini chanzo cha moto huo uliozuka siku ya ijumaa kwenye jengo hilo ambalo lilikuwa limezeeka na ambalo liligeuzwa kuwa studio ya muziki. Inasemekana kuwa hakukuwa na kibali cha jengo hilo kutumika kama makazi ya binadamu au hata eneo la burudani.





Tumerekebisha ....endelea kutuamini. (Mhariri)

Post a Comment

 
Top