0


--------------------------------------------------------------------------------------
Baadhi ya wanasheria kutoka nchi za ukanda wa Afrika mashariki  na maziwa makuu ikiwemo Burundi, Rwanda na DRC watembelea ofisi za Umoja wa nchi za Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha katika hatua ya mafunzo ya kuongeza na kujenga uwezo (Building Capacity).
--------------------------------------------------------------------------------------



Wanasheria na majaji kutoka nchi za ukanda wa afrika mashariki na maziwa makuu, wakiwa katika kikao cha kwanza wakimsikiliza Katibu mkuu wa ABA–ROLI Fabien Kazamira alipokuwa akiongea namna ya kujengewa uwezo na kujifunza jinsi umoja wa nchi za Africa unavyofanya kazi, kikao hiki muhimu kilifanyika kwenye Hotel ya African Tulip jijini Arusha.

Claudine Umugwaneza akichangia jambo wakati wa kikao cha kwanza huku akiongea kwa mkazo kuhusu sheria za nchi moja moja zinavyoweza kuwa kikwazo kwa wananchi wa jumuiya hii ya EAC.

Mjumbe katika kikao hicho ambaye pia ni mwanasheria kutoka Burundi Muhezenge Jean de Dieu akimsikiliza kwa makini maelezo ya Claudine. 
Baada ya makubaliano yaliyomalizika katika kikao cha siku moja, walipiga picha ya pamoja kuweka kumbukumbu kwa ajili ya mafunzo hayo, aliyekaa mkono wa kushoto ni Odette Ntahiraja ambaye ni mwakilishi Mratibu wa kwanza aliyesimama kulia ni Louis Marie Nindorera –Mkurugenzi mkaazi na Mipango wa kanda.
Majaji na wanasheria kutoka Burundi, Rwanda na DRC wakifurahia jambo kutoka kwa Ofisa wa nchi wanachama za Afrika mashariki ambaye ni Mtafiti mchambuzi Dr. Fabien Ngendakuriyo hayupo pichani alipokuwa akieleza namna nchi hizo zilivyo na nafasi kwa raia wake kufanya biashara pasipo bugudha
Dr. Fabien Ngendakuriyo kulia aliyeshika tama akiwa makini kumsikiliza ofisa mwenzake G. Kazinduka wa ofisi za Umoja wa Afrika Mashariki alipokuwa akiongea na wanasheria, majaji waliotembelea Ofisi za umoja huo (hawapo pichani) jinsi wanavyotekeleza majukumu yao.
Rais au Mkurugenzi wa mipango wa kanda Louis Marie Nindorera kushoto akiteta jambo na Ofisa wa sekreterieti ya EAC Kazinduka mara baada ya kumaliza kusikia kazi wanazofanya makao makuu ya umoja wa nchi za Afrika Mashariki jijini Arusha.
Maofisa wa sekretarieti ya umoja wan chi wanachama za afrika mashariki pamoja na wanasheria, majaji waliotembelea ofisi za umoja huo zilizopo jijini Arusha wakimsikiliza Katibu mkuu wa ABA Fabien K. Kazamira (hayupo pichani) alipokuwa akiuliza swali kwa maofisa hao watatu wa kwanza wa pili na watatu mkono wa kushoto.
Eneo lililopo ndani ya jengo la makao makuu ya Afrka mashariki penye picha mbalimbali zenye matukio ya viongozi wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika mashariki lililomvutia Odette Ntahiraja (kushoto) Mratibu wa American Bar Association na Claudine Umugwaneza na kupiga picha.
Vilevile walipata nafasi ya kupiga picha ya kumbukumbu wakiwa pembezoni mwa ofisi za EAC jijini Arusha kuashiria kupata mafunzo yaliyowajengea uwezo na kutambua kazi mbalimbali zinazofanyika katika ofisi hizo kuu kwa ukanda wa nchi za jumuhiya hizo.



HABARI KWA UFUPI:

Wakiwa katika mkutano mdogo walioufanya katika hotel ya African Tulip na kisha kuelekea kwenye ofisi kuu za ushirikiano wa Afrika mashariki kupata uzoefu kwa wanasheria, maofisa na watendaji wa makao makuu hayo, wanasheria hao na majaji wameona nia ya msaada kutumika kwa ukanda huo..

Matatizo ni mengi pamoja na kuwepo na wakata miti, shule kufuata utaratibu mmoja lakini kuna nchi zina uhuru ikiwemo Tanzania ambapo unaweza kufanya biashara ukiw huru kabisa iwe ni mayai, kuuza karanga popote inawezekana, hali hii pia ipo katika nchi nyingine za ukanda huo lakini ni jambo linalohitaji ushirikiano zaidi, anasema Dr. Fabien Ngendakuriyo.
  
Mkutano wa wanasheria na mahakimu kutoka nchi za ukanda wa Africa mashariki na  maziwa makuu pia walijadiri mahusiano ya sheria zinavyoweza kushirikisha ukanda huo, huku wakitazamia wananchi wote wafaidike na umoja huo ikiwepo kuwepo kwa usawa kwa wananchi wote wa ukanda huu kama kuwapa usawa kwa pande yoyote iliyopo ndani ya umoja huo pasipo kubagua.

Post a Comment

 
Top