0


Akiwa ni kijana wa aliyezaliwa kutoka katika familia ya wakulima wa miwa nchini cuba, Fidel Castro alizaliwa mnamo mwaka 1926, ambapo wakati wa uhai wake alimuoa mke wake ambaye alikuwa ni msaidizi wa ndani (housemate) ambaye baadaye alimuoa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja aitwaye Fidelito, hata hivyo ndoa yao haikudumu.




Fidel Castro enzi za uhai wake.

Akiwa kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya kikomunisti, Fidel Castro alifanikiwa kuibuka kuwa mwanasheria na mwanamapinduzi nguli wa muda mrefu, ambapo baadaye alaikamatwa kwa jaribio lililoshindwa la kuiangusha serikali ya kiongozi wa wakati huo Fulgencio Batista, kufuatia kitendo hicho alihukumiwa kifungo kilichomsaidia kumpa umaarufu cha miaka 15.




Wananchi wa Cuba mara baada ya kupokea taarifa za kifo cha Fidel Castro walikusanyika kwa wingi.

Rais Raul Castro wa cuba ambaye ni ndugu wa marehemu Fidel Casrto alitangaza kifo cha ndugu yake huyo aliyekuwa amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba na alitawala kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kaka yake Raul kuchukua madaraka mwaka 2008 kuwa amefariki dunia akiwa na miaka 90 majira ya saa 22:29 usiku huu wa kuamkia leo jumamosi.

Enzi za uhai wake aliwahi kukiri kwamba umri ulikuwa umempa mkono na kwamba amezeeka sana lakini alisema maadili ya kikomunisti kwa wacuba bado yana maana na kwamba raia watashinda, alikabidhi madaraka kwa muda kwa kakake mwaka 2006 alipokuwa anaugua maradhi ya utumbo hata hivyo Raul Castro alikabidhiwa rasmi madaraka ya urais miaka miwili baadaye 2008.


  FIDEL CASTRO 1926 -2016  
Akikaribia kutimiza miaka 90 Rais huyo wa zamani alipata kusema katika hotuba yake ya mwisho 19.4.2016 alipokuwa akiwaaga wafuasi na wanachama wa kikomunisti kwamba ni “jambo ambalo sikuwahi kulifikiria lingetimia,hivi karibuni nitakuwa kama hao wengine, kwetu sote lazima wakati wetu utafika ". Wafuasi wake wanasema alikuwa ameirejesha Cuba kwa wananchi pamoja na kutuhumiwa kuwakandamiza wapinzani. Pia alisema "ingawa nitatoweka duniani lakini mapinduzi yataishi milele”.

Itakumbukwa kuwa chini ya uongozi Cuba ilikuwa na uhusiano mzuri na mataifa kadhaa ya Afrika, ikikumbukwa miaka ya 1970 na 1980 ambapo maelfu ya madaktari na walimu kutoka Cuba walikuja barani Afrika na idadi sawa ya askari pia walisafirishwa kuja kuingilia kati migogoro kutokana na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.


>>.................................................................................................HISTORIA YAMUANGAZIA FIDEL CASTRO:

§  1926: Alizaliwa mkoa wa kaskazini mashariki wa Oriente nchini Cuba.
§ 1953: Alifungwa jela baada ya kuongoza maasi ambayo hayakufanikiwa dhidi ya utawala wa Fulgencio.
§  1955: Aliachiwa huru kutoka jela chini ya mkataba wa msamaha.
§  1956: Akiwa na Che Guevara, alianza vita vya kuvizia dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani.
§  1959: Amshinda Fulgencio Batista na kuapishwa kuwa waziri mkuu wa Cuba.
§  1961: Aliwashinda wapiganaji waliofadhiliwa na CIA waliovamia Bay of  Pigs
§  1962: Alianzisha upy mzozo wa makombora wa Cuba kwa kukubali Urusi ya wakati huo USSR iweke makombora Cuba.
§  1976: Alichaguliwa kuwa Rais na Bunge la Cuba
§  1992: Aliafikiana na Marekani kuhusiana na wakimbizi wa Cuba
§  2008: Aling'atuka madarakani kwa sababu za kiafya.
§  2016: Historia yake yafungwa rasmi hapa duniani.


Post a Comment

 
Top