Chama cha wanawake
wajasilamali nchi TWCC kimefanya mkutano wa kiuwezeshaji unaolenga kupunguza
changamato wanazokumbana nazo katika biashara za ndani na nje ya mipaka ya
nchi, ambapo imeonekana kuwepo kwa changamoto nyingi ikilinganishwa na wakati
wa huko nyuma.
Hata hivyo miongoni mwa
changamoto hizo zinazoainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho Jackeline Maleko
anasema “asilimia zaidi ya sabini ya
wafanyabiashara wanofanya biashra mipakani ni kinamama, kutokana na hilo ili
kuwawezesha wafanye biashara kiushindani na kiuhakika, tumeona tuwafuate pale
walipo na kujua wapi panapowazuia kufikia malengo”
Vilevile pamoja na
vikwazo hivyo wanavyokumbana navyo vinaweza kuondolewa endapo wahusika wataona
jitihada za wafanyabiashara hao kufikia masoko makubwa ambapo watakuwa
wamekidhi vigezo.
Vigezo vinavyoweza
kufikia malengo makubwa ni pamoja na kupata cheti kutoka taasisi zinazotambua
ubora wa bidhaa kama TBS, TFDA n ahata nembo ya utambuzi wa garama ya bidhaa ‘Barcode’.
>>Habari hii unaweza kuiangalia kupitia HABARI KATIKA VIDEO mwanzo wa ukurasa.
Post a Comment