0

Muundo wa aina ya njia ya treni ya kisasa ujulikanao kama Standard Gauge unavyoonekana.

Shirika hodhi la rasilimali za reli nchini, kupitia kwa mkurugenzi wake Dkt. Mussa Iddi Mgwatu ambayo ndiyo inatekeleza na kusimamia ujenzi mkubwa wa reli ya kisasa nchini ambao unatarajiwa kutumia kiwango cha Standard Gauge, ambayo itakuwa na uwezo wa kwenda km120 kwa saa, unatarajiwa kuanza hivi karibuni, ukianza kujengwa kilomita 1,219 ikitarajiwa kugharimu kiasi cha shs bilioni 3.694.



Mkurugenzi mkuu wa Rahco nchini Dkt. Mussa Iddi Mgwatu
Wakati wananchi wakiwa na matarajio mengi kutokana na mradi huu mkubwa mara utakapokamilika, mkurugenzi wa RAHCO anasema, wanatarajia kununua injini mpya na mabehewa ya mizigo na abilia, ambapo mradi huu hautaingiliana na ule wa TRL wa sasa, amabpo huu mpya utaleta manufaa mengi ya kiuchumi na kijamii ikiwa ni kuboresha usafirishaji hata kwa nchi zisizokuwa na bandari kuelekea masoko ya Afrika na Dunia kwa ujumla.

Wakati huo huo, ujenzi wa reli kwa kiwango hiki cha Standard gauge utafanywa kutoka Dar kwenda Mbamba bay, Tanga kwenda Arusha na Musoma, mipango yote hii ipo katika upembuzi yakinifu na mingine tayari.


 Lakini pia ujenzi katikati ya jiji la Dar Es Salaam kwa ajili ya kupunguza msongamano pia utajengwa ili kuleta maendeleo kwa watanzania kupitia sekta muhimu ya usafirishaji.

Post a Comment

 
Top