Tunaomba radhi kwa kutokuziweka wazi picha za tukio hili moja kwa moja hapo chini kutokana na muonekano wake kuogofya lakini pia kulinda na kutunza utu.
Eneo ambalo tukio hilo
limetokea huko magharibi mwa Uganda likionekana kwa mbali.
|
Mmoja wa watuhumiwa ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uganda |
Hizi ni moja ya picha za
tukio hilo la kuogofya ambazo zinasikitisha.
|
Hii ni moja ya picha za tukio hilo la
kuogofya ambazo zinasikitisha.
|
Sehemu ya watu waliopatwa na janga
kutokana na tukio hilo la kuogofya linalosikitisha.
|
HABARI ZAIDI:
Kulingana na taarifa za
vyombo vya habari zilizotoka muda mfupi uliopita maofisa wa polisi
wamesema tayari idadi ya watu waliouawa katika mapigano hayo imefika watu
62.
Maafisa wa polisi
walikabiliana na wapiganaji wanaotaka kujitenga waliopo magharibi mwa taifa
hilo, ambapo mfalme wa Rwenzururu, Charles Wesley Mumbere, amekamatwa na kupelekwa katika mji mkuu wa nchi hiyo
Kampala, akituhumiwa kwa kuchochea ghasia, lakini amekana mashtaka hayo pamoja
na kukana kumiliki wapiganaji na kuchochea ghasia.
''Tunataka miili ya
watu wetu ili kuwapatia maziko ya heshima, baadhi ya miili ipo katika lango la
jumba la mfalme huyo na haturuhusiwi kuingia'', alisema Joy Biira mwanahabari wa kituo cha runinga ya KTN nchini
Kenya ambaye alikamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa usalama wa nchini Uganda
usiku wa Jumapili iliyopita.
Vyombo vya habari
vinasema mwanahabari huyo alikamatwa pamoja na wengine watano kwa
tuhuma za kupiga picha na video kuhusu operesheni ya maafisa wa usalama katika
kasri la mfalme wa Rwenzururu na kuzichapisha kwenye mitandao ya kijamii, hata
hivyo wanahabari na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wametoa wito kwa
serikali kumwachilia huru mwandishi huyo.
Post a Comment