Faraja Kota Akikaribisha wageni katika kongamano la kinamama la siku 16 za kupinga uonevu dhidi ya mwanamke unakoma. |
Wana-kongamano
waliohudhulia kongamano la wanawake kitaifa lililofanyika jijini Dar Es Salaam
katika ukumbi wa kimataifa wa Kisenga LAPF wakisikiliza mada kutoka kwa viongozi watendaji.
|
Mtendaji
mkuu Taasisi ya kisheria ya wanawake Tike Mwambipile ambaye akitanabaisha
Malengo ya kongamano hilo ambalo linawaleta
wanawake wote nchini kujadiri na kuona jinsi ya kutatua changamoto zao..
|
Baadhi
ya wanawake waliohudhulia kongamano la wanawake kitaifa lililofanyika jijini
Dar Es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Kisenga LAPF wakisikiliza mada
kutoka kwa wageni.
|
Baadhi
ya wanafunzi kutoka chuo cha ufundi Temeke walioudhulia kongamano hilo ili
waweze kujifunza na kupata hamasa kuhusu haki zao zitakazowafanya kuvuka hatua
moja kwenda nyingine.
|
Mama
Kejo Bisimba kushoto mkurugenzi wa (LSF) Kess Greonerndijk kushoto na katikati
ni Edda Maliki wakiteta jambo mara baada ya mapumziko mafupi wakati wa
kongamano hilo.
|
HABARI KWA UNDANI:
Sheria inalenga kuweka uhuru na haki kwa kila mtu ili asiweze kuonekana na kosa lakini pia inalenga kutoa haki sawa kwa kila binadamu.
Serikali imeshauliwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za kisheria jambo ambalo litasaidia kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake hususani suala la ukatili wa kijinsia ambalo limekuwa sugu katika mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la kitaifa la haki za wanawake spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Anna Makinda amewataka wanawake kujitambua na kuijua sheria ili wapate nguvu ya kujitetea itakayowasaidia kupata haki zao.
Hata hivyo ameiomba serikali kufanya jitihada kubadirisha sheria ya mwaka 1971 kutokana na sheria hiyo kuwabeba wanaume katika masuala mazima ya haki ikiwemo mirathi, vilevile amesema wanawake wana matatizo ndani ya Ndoa hivyo kuna umuhimu wa kuweka sawa ili kuondokana na matatizo yanayoweza kujiutokeza.
Na ikiwa ni kumuwezesha mwanamke kujitambua, Sheria na huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja mambo yuanayomnyima mwanamke maendeleo pamoja na kumuwezesha mwanamke kielimu na kupitia taarifa.
Kituo cha huduma za haki kisheria nchini (LSF) mara kadhaa kimekuwa mstari wa mbele kuwawezesha wanafunzi ikiwemo wale wanaoshindwa kutimiza malengo yao kama wanafunzi wasio na uwezo wa kufikia matamanio ya mafanikio kielemu hususani waliofiwa na wazazi wao na kukosa mlezi wa kumpa nafasi kusoma.
Mwanamke anapaswa kuwezeshwa kuhusiana na haki zake, ajitambue, ajiamini na asimamie haki yake.

Akitoa moja ya unyanyasaji aliowahi kushuhudia katika mkoa mwanza huko ukerewe Spika huyo mstaafu anasema, "kuna kitendo cha mwanamke kutakaswa pale anapofiwa na mumewe, hii ni tabia mbaya sana inapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote", pamoja na hilo amegusia tabia ya wanaume wa mkoani Iringa ambao uwaambia wake zao wanapokuwa wananyonyesha wasiwanyonyeshe watoto moja ya ziwa ili atokapo kulewa naye aje anyonye ili kupunguza pombe aliyokunywa!!.

Post a Comment