Wagombea wawili wanaopigania kura kutoka kwa raia wa marekani ni Donald Trump wa chama cha Republican na Bi Hillary Clinton wa chama cha Democratic.
Taarifa zinaeleza zaidi kuhusu bwana Trump wakati akipiga kura kuwa;
Alifika katika kituo cha kupigia kura Mashariki mwa mji wa Manhattan akiandamana na mkewe Melania, binti yake pamoja Ivanka ambaye ni shemeji yake
"Ni kwa heshima kubwa, alisema huku akipiga kura, ifanye Marekani kuwa tukufu tena," hayo ni maneno ya Donard Trump alipokuwa anawaambia wapiga kura mapema leo.
Wakati huo huo Chansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel amesema kuwa ushindi wa Hillary Clinton utatoa muelekeo wa kuwepo usawa wa kijinsia miongoni mwa viongozi wa dunia.
"Hakika tutakuwa karibu hata kuwepo kwa usawa kati ya wanaume na wanawake katika nyadhifa za juu". Hayo n maneno ya Chansela huyo ambaye ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini Ujerumani, ambapo alikuwa akiongea mjini Berlin akiwa na Erna Solberg, ambaye ni waziri mkuu wa pili mwanamke nchini Norway
Mpaka tunapokuletea habari hii wananchi wa taifa hilo kubwa duniani na lenye nguvu wanaendelea kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura, itakayowapelekea kuingia kwenye historia kumpa wadhifa huo mkubwa mwanamke wa kwanza kukalia kiti cha white house ya marekani hama kumpa Donard Trump mtu anayetazamwa kuwa machachari katika dunia.
NOTE: Fuatilia habari za uchaguzi huu hapa hapa kupitia http://todayspro.blogspot.com mpaka matokeo ya mwisho....
Post a Comment