0


Wachezaji wa Tanzania wakiwa katika mazoezi kabla ya mchezo wao usiku wa kuamkia jumapili huko india.
Timu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioambana nao katika mashindano hayo, hapa ni kabla ya mchezo na Irani.
Timu ya Irani katika picha ya pamoja na viongozi wao kabla ya mchezo wao na timu ya Tanzania.




Michezo ya kombe la dunia inayoendelea kwenye nchini india katika jimbo Punjab, timu za Tanzania zilizoelekea katika mashindano hayo mpaka sasa bado hazijaonyesha makeke yake kutokana na mechi za awali walizocheza mpaka mwishoni mwa wiki hii.

Katika michezo miwili ya mashindano hayo ya dunia waliyocheza, ikiwa mchezo wa kwanza uliochezwa Novemba 04 kati ya Tanzania na Argentina, matokea yalikuwa timu ya Argentina52 na Tanzania32 ikiwa ni ushindi wa point 20.

Mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo kwa saa za india 16:30  kati ya Tanzania na Iran, mwanzo mwa mchezo ilionekana  kuwepo kwa ushindani, lakini kadiri mchezo ulivyokuwa unaendelea wachezaji wa timu ya Tanzania walionekana kuzidiwa kutokana na timu timu ya Iran kuonekana wana nguvu na wameshiba kulinganisha na wachezaji wa Tanzania.


Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Wanaume wakiwa gym wakijifua. 

Katika mchezo huo matokeo yalikuwa Irani65 na Tanzania23 huku ikionyesha Tanzania kunyukwa kkwa point 42. Mpaka sasa timu hiyo imecheza mechi mbili, haijashinda, imepoteza mechi mbili na haijapata suruhu, Wachezaji wa timu hiyo walikuwa Gasper Joseph, Robert Ephraim, Ramadhani Juma, Benjamin Michael, Amos Kamani, Musa Kagoma, Michael Thomas, Kidai Joseph, Charles Caphason na kepteni Shija Shingamagaji.



Picha by Issa Ndokeji/ITV

Post a Comment

 
Top