Mtaalam wa lugha, mafunzo ya kusikia na vifaa
pandikizi, Fayaz Jaffer akiongea katika
hafla ya kuhitimisha siku sita za utolewaji wa mafunzo kwa wataalam kutoka nchi
kumi na moja mapema wiki j-hii jijini Dar Es Salaam.
Fayaz Jafar watatu kutoka kushoto na mkewe aliyepokea
vyeti akiwa ni mmoja wa walioshiriki mafunzo hayo wakiwa na wakufunzi pamoja na
mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya taifa ya muhimbili.
|
HABARI KWA UNDANI
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPORT.COM
Kwa mara ya kwanza katika historia ya bara la
afrika, Tanzania inaigia katika historia kuwa nchi inayoweka/kupandikiza kifaa cha
usikivu kinachoweza kumfanya mtu asiyesikia aweze kusikia unaenda kufanyika
nchini Tanzania huku madaktari wazalendo wakihusika moja kwa moja katika
hutoajihuo wa huduma.
Katika mafunzo ya siku sita yalifanyika jijini Dar
Es Salaam na kuendeshwa na wataalam kutoka nchini Australia yalishirikisha
zaidi ya nchi 11 kutoka za Africa, ambapo
mafunzo hayo yamelenga kuwapa wataalam hao ujuzi na njia zitakazoweza
kuwasaidia katika kufanikisha utoaji wa huduma hii.
Wakati mafunzo hayo yamewahi kufanyika katika nchi
nyingine kama Misri na kushirikisha wataalam kutoka nchi nyingine za afrika, kwa
sasa Tanzania ndiyo itakuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hii huku serikali
ikuhusika moja kwa moja ili kuwezesha huduma kufanyika kwa ukaribu. Ambapo
mafunzo hayo yamelenga kuandaa mazingira na lugha, ikiwa ni asilimia 80% ya
huduma .
“Upandikizaaji wa kifaa hicho umekuwa
ukitolewa na wataalam wa kutoka mataifa ya ulaya huku garama zake zikiwa juu na
pale unapohitaji kwa mfano kuongeza wigo wa usikivu kwa yule aliyepandikizwa au
marekebisho yoyote inampasa kufunga safari kwenda kwa daktari wake ulaya, hivyo
kwa sasa huduma hii inaenda kufanyika hapa nchini, huku nchi jirani zikija
kupata huduma na uzoefu zaidi” anasema Fayaz Jaffaer mtaalam wa
kifaa usiku kwa wasiosikia.
www.youtube.com/embed/qdObHkJmoSY
https://youtu.be/qdObHkJmoSY
Wale wasio sikio kuna sababu kubwa tatu zinazofanya
mtu asiweze kusikia, maana sikio limeganyika katika sehemu tatu, kuna sehemu ya
nje, katika na sehemu ya ndani, wale wasiosikia kuna sehemu ya ndani
ijulikanayo kwa jina Cochlear Implants inakuwa imeathilika hivyo basi
upandikizaji wa kifaa hiki kinaenda kusaidia kufanya kazi badala ya vile viini
vilivyokufa hivyo mtu asiyesikia anaweza kusikia.
Daktari bingwa wa magonjwa ya masikio Edwin Liongo
wa hospitali ya Taifa ya muhimbili anasema, “mara nyingi
mtoto aweze kuongea lazima asikie na kuna watoto wanaozaliwa wanakuwa hawaongei
na wazazi hawajui ni kwa nini, na wengine hudai mtoto kaachewa kuongea mpaka
inafikia miezi tisa ambayo mtoto anapaswa kuanza kuongea, lakini ikifika mpka
hatua hiyo bado basi anaweza kuwa ana tatizo la kutokuongea hivyo kifaa hiki
kinapowekwa kinamuwezesha mtoto na kupata mawasiliano ya moja kwa moja”.
Mtoto anapewa nafasi kubwa kupata upandikizaji huu
kutokana na maumbile yake bado yana nafasi na uwezo mkubwa kupokea mafunzo na
muongozo mpya uliopo mbele yake kulinganisha na mtu mzima, hivyo inapofungwa
inawashwa kwa sauti ndogo na kila baaada ya muda uongezwa kutokana na mazoezi
anayopewa na mtaalam mwenye uzoefu na kifaaa hicho.
Unaweza kuangalia habari hii zaidi kupitia NEWS news
video katika blog yetu muda ujo.
Post a Comment