![]() |
| Mzee Samweli Sitta enzi za uhai wake. |
Kilichojiri kwa ufupi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa spika
wa bunge la tisa la Jamhuri la muungano makao makuu ya nchi mjini Dodoma katika ukumbi wa bunge alasiri ya leo.
![]() |
| Jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa Karimjee |
NAIBU SPIKA: Tulia Atickson ambaye ni naibu spika alisimama
na kutoa hotuba kwa niaba ya spika wa bunge la sasa John Ndugai ambapo aliweza
kuelezea hatua zote za maisha alizopitia mpaka kifo chake huko nchini Ujerumani
alipokuwa akipewa matibabu.
Marehemu Samwel Sitta ameacha mjane ambaye ni mbunge
wa urambo mashariki mama Magreth Sitta ambaye walifunga naye ndoa mwaka 1969,
na ameacha watoto watano, pia alichaguliwa kuwa spika wa bunge mwaka 2005
ambapo aliweza kuongoza bunge lililokuwa na speed na viwango kama alivyotamka
mwenyewe.
![]() |
| Rais mstaafu Jakaya Kikwete akitoa heshima pembeni ya jeneza. |
ZITTO KABWE: Pamoja na salamu za upinzani, huku
akimtaja kuwa mwanachama kindani wa timu ya simba, alisifu juhudi za marehemu
Samweli Sitta akisema alikuwa spika wa watu amabaye aliboresha bunge kupitia
uhuru wa kutoa michango bila kubagua vyama, pia alianzisha mfuko wa majimbo, kutetea
mkoa wa Tabora na aliwafundisha wabunge namna ya kujibu maswali wawapo bungeni.
TUNDU LISSU: Alianza kwa kumtaja marehemu kama
mwamba wa miamba wa bunge, ambaye hakuna kama yeye, ambapo alilifanya bunge
kufahamika ndani na nje ya mipaka ya taifa, ikiwa na kulitaka bunge kuwa lenye ‘meno’
uwezo katika maamuzi, likiwa linaisimamia serikali ipasavyo katika uendeshaji
wa serikali na ameliweka bunge kwenye ramani ya Tanzania.
SAMSON RWEKIZA: Ambaye ni katibu wa bunge anasema
alijuana na marehemu na akiwa kama mzee mwenye hekima na ndiyo maana akapata
kufika katika ngazi za juu serikalini.
FREEMAN MBOWE: Kambi ya Upinzani, tulimuona mzee
sitta kama kiongozi ambaye hana ubaguzi wa kiitikadi ambaye alisikiliza makundi
yote, vilevile alipigania kile alichokiamini, akitetea upinzani wa pale
alipoona hapakuwa sawa aliweza kukosoa na pale alipoona serikali inaonewa
alikuaw tayari kuitetea.
WAZIRI MKUU: Kassim Majaliwa kabla ya kuhitimisha
kazi za bunge alitoa salamu zake alisema marehemu Samweli Sitta alikuwa
kiongozi mlezi, mwadilifu, mwenye kuimarisha demokrasia na msema ukweli. Aliweza
kuunganisha watu wote na alikuwa mtumishi wa kila mtu, Bwana ametoa na Bwana
ametwaa Jina lake na libalikiwe.
SPIKA WA BUNGE: John Ndugai ambaye ndiye spika
aliyechukua mikoba ya uspika mara baada ya marehemu mzee Sitta kustaafu nafasi
hiyo alisema; Samweli Sitta alisimamia bunge vizuri, pia aliunda bunge
linaloisimamia serikali na kuthibiti, lakini pia katika kulitengeneza bunge la
tisa ambapo bila kuwasahau wabunge waliomsaidia kulisaidia bunge katika
utendaji kama Ndugai, Mwakyembe, Mhagama, Dr. Slaa na wengine.
Kwa mara ya kwanza aliunda kamati ambazo nyingine
zilikuwa na wenyeviti kutoka vyama vya upinzani ili kuonyesha uwajibikaji
katika shuguli za bunge.
Kisha mwili wa marehemu ulikuwa tayari kwa ajili ya
safari ya mwisho kupelekwa mkoani Tabora kwa ajili ya kuhifadhiwa katika nyumba
ya milele.
Dawati
la habari kutoka TODAYSNEWS Blog linawapa pole ndugu jamaa na watanzania wote
kwa tukio hili.



Post a Comment