![]() |
Nembo ambayo itatumika kulitambulisha shirika
litakalokuwa linashugulika na afya ya mama na mtoto, linalojulikana kwa jina la
Thamini Uhai.
|
![]() |
Bendi ya muziki ya Wahapahapa ambayo ilikuwepo
kutumbuiza muziki wakati wa uzinduzi rasmi shirika Thamini Uhai mapema katika
hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jijini Dar Es Salaam.
|
HABARI KWA UNDANI:
Shirika la Thamini Uhai
limezinduliwa rasmi leo jijini Dar Es Salaam, shirika hilo ilinalojishugulisha
na uokoaji, uboreshwaji wa mazingira na maisha ya wanawake kupata huduma nzuri
na zenye ubora kwa uzazi hasa za dharula katika maeneo ya vijijini na maeneo
yaliyosahaulika.
Thamini uhai inaweza
kujihusisha na uhifadhi ikiwa ni pamoja na kuonyesha idadi ya mambo
yaliyomalizika kijiografia, vituo vya afya na hospitali katika wilaya nane
mkoani kigoma na pwani tangu mwaka 2008. Kufikia hatua hiyo ya uboreshwaji wa
maisha ya mama na watoto wachanga kwa kushirikiana na serikali.
Wakati wa utambulisho
rasmi wa jina Thamini Uhai, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dr. Mwakatundu
amesema chimbuko lake limetokokana na shirika la kimataifa la World Lung
Foundation ambalo limekuwa likifanya kazi kwa karibu sana na serikali katika
jitihada za kupunguza vifo vya kimama na watoto wachanga tangu mwaka 2008
mkoani kigomma na Pwani.
Wakati shirika hilo
likiwa na ushirikiano na serikali pamoja na wadau wengine ikiwa ni kuboresha
uwezo na upatikanaji wa huduma timilifu za dharula na uzazi, (COMPREHENSIVE EMERGENCY
OBSTRETIC NEONATAL CARE) katika vituo vya afya 19 kwenye maeneo yaliyosahaulika
pia imesaidia upatikanaji wa wataalam wenye ujuzi wa juu kwenye uzalishaji wa
huduma za dharula.
Hata hivyo mgeni rasmi
ambaye ni mwakilishi kutoka hospitali ya muhimbili Dr Winani alisema, katika
muongozo wa serikali ambao unalenga kumfanya mtanzania asiweze kutembea zaidi
ya kilomita 5, kuwepo na mtaalam mzoefu atakayehudumia kituo husika ili
kusaidia upatikanaji wa huduma za kitaalam.
Naye mkurugenzi wa
White Ribbon Allience Tanzania Rose Mlay amesisitiza kuwa mara kadhaa bajeti ya
vituo vidogo vya afya ambavyo uanzishwa na mashirika mara kadhaa imekuwa ni
fedha ya wafadhili ambayo uishia katika uanzishwaji wa vituo hivyo lakini pesa
ya uendeshwaji utoka serikalini, lakini serikali utoa pesa pale panapoonyesha
kufanya vizuri.
Mjadara kuhusu hali ya
afya kwa mama na mtoto inachagizwa kwa wananchi kutambua nafasi ya kila mtu
analindwa na mfumo imara wa afya kwa umma, kabla ya hapo inafahamika wagonjwa
walikuwa wakikimbizwa hospitali kwa saa tatu au nne kwa hospitali ya karibu,
mpaka sasa dharula huduma ya uzazi inapatikana katika jamii.





Post a Comment