Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi nchini Godfrey
Simbeye akifafanua jambo.
|
Leonard Mutani.
TODAYS NEWS.
Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa
ishirini moja wa kimataifa wa wajasilia mali wadogo na wakati unaotarajia
kufanyika mnamo mwezi wa 12 tarehe 5 hadi saba mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar Es Salaam
mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi nchini Godfrey Simbeye amesema
kupitia kongamano hilo litakalo wakutanisha washiriki kutoka mataifa
mbalimbali, litasaidia kuitangaza nchi kimataifa.
Pia alisema mkutano huo ambao kwa mara ya kwanza
unafanyika katika ukanda wa afrika ya mashariki hivyo kuwa wenyeji wa mkutano
huo, utaisaidia kuitangaza nchi kimataifa hasa fursa zilizopo hasa katika hazma
ya kufikia nchi ya viwanda na muunga mkono Rais John Magufuli katika hazma yake
ya kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa viwanda.
Adha bw Simbeye aliongeza kuwa kupitia mkutano huo washriki watapata
nafasi ya kukuza wigo wa mtandao ya kibiashara hasusani kwa makampuni ya ndani kwa
pamoja na kubadilishana uzoefu, sambamba na kutangaza bidhaaa zinazozalishwa na
viwanda vya ndani.
Mkutano huo ambao umeandalia kwa ushirikiano kati ya
taasisi ya sekta binafsi nchini kwa kushirikiana na AICC –JNICC pamoja na
taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi kama wizara ya Viwanda na Biashara,
SIDO, TIC, EPZA, ZIPA, TTB NA TAN-TRADE.
Post a Comment