|
Mwananchi akiwa katika kambi mara baada ya makazi yao
kukumbwa na dhahama ya mafuriko nchini humo akijishugulisha na upepetaji wa
chakula.
|
Kumekuwepo na mikutano mikubwa kadhaa barani
Afrika inayolenga kuangalia ni njia gani inayoweza kusaidia kupunguza ukosefu
wa chakula hama kuongeza upatikanaji wake ili kufidia mapungufu yanayojitokeza
mathalani katika baadhi ya nchi zinazokumbwa na janga la njaa.
|
Rais wa Malawi Peter Mutharika |
Nchini
Malawi Rais Peter Mutharika amesema nchi yake hivi sasa imepata chakula cha
kutosha kinachoweza kulisha nusu ya idadi ya watu nchini humo ambao walikuwa
wanahitaji msaada wa chakula.
Akilihutubia taifa kwa mara ya pili tangu mwezi mei mwaka huu, amesema anafahamu maumivu wanayokabiliana nayo wananchi wengi na anaelewa kwamba kuna hali ya kutokuwa na uvumilivu wa kuondokana na changamoto zinazowakabili kwa sababu taifa linaathiriwa na umaskini wa miaka mingi.
|
Wananchi
wakipita katika moja ya maeneo ya mashamba yaliyokumbwa na ukame kutokana na
uhaba wa mvua mara baada ya mvua za El nino zilizopelekea uharibifu wa mazao na
maeneo kukosa mvua za kutosha na kupelekea kukausha mazao.
Nchi
ya Malawi imekumbwa na tatizo kubwa la ukosefu wa chakula tangu kuwahi kutokea
kwa muongo mzima uliopita. Watalaamu wa masuala ya hali ya hewa na kilimo wanasema
hali hii kwa kiasi kikubwa imetokana na mvua za El Nino ambazo zimesababisha
ukame na mafuriko ambayo yameathiri mazao kwa miaka miwili iliyopita.
Ripoti
ya hivi karibuni kutoka kwa kamati ya tathmini imeonyesha kwamba wananchi zaidi
ya milioni 6.5 ambayo ni sawa na nusu ya idadi ya wananchi wote wa Malawi, wamekumbwa
na njaa hivyo kupelekea kuhitaji msaada wa chakula.
|
Post a Comment