0


Wakulima kadhaa wa bustani za mbogamboga nchini wamekuwa wakilima na kuvuna mazao yatokanayo na bustani kama mbogamboga, matunda, maua na viungo visivyo salama kutokana na mazingira wanayolima kutokuwepo kwa mahitaji  muhimu ikiwemo upatikanaji wa maji salama kwa mimeo ya bustani pamoja na matumizi ya madawa.




Baadhi ya wataalam na wadau wa kilimo cha mbogamboga kutoka mikoa kadhaa jirani na mkoa wa Arusha wakifuatilia mada kutoka kwa Stephern Kijazi alipokuwa anachangia, mkutano uliofanyika katika hotel ya Arusha Hotel jijini Arusha.

Mdau wa kilimo cha mbogamboga na matunda Stephen Kijazi akigusia njia bora za uzalishaji  wa mazao unavyoweza kutoa mazao bora maana ujuzi na maarifa unahitajika katika kuzalisha mazao hayo.

Picha yenye kuvuta hisia kwa mmoja wa wadau kushika shavu alipokuwa akimsikiliza mmoja wa wachangiaji ndg ndg Merius Nzalalawale ambaye alitoa mada yenye kuvuta hisia tofauti.



HABARI KWA UNDANI:
Leonard Mutani -Arusha        

Kufuatia uzalishaji wa mboga zisizo na viwango taasisi isiyo ya kiserikali ya nchini Netherlands ya Solidaridad imewakutanisha wadau wa kilimo cha mbogamboga za bustani pamoja na matunda kuweza kuangazia jinsi gani kutakuwa na uwezekano wa kupata mazao yatokanayo na bustani yaliyo salama kwa matumizi ya binadamu, mkutano huo umefanyika jijini Arusha na kuwakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi zinazojikita katika ukulima wa bustani za mbogamboga na matunda.

“kumekuwa na changamoto kwa Tanzania baadhi ya mbogamboga zimekuwa zikilimwa sehemu ambazo si salama, maeneo ambayo yanatiririka maji kutoka viwandani na baadhi ya wakulima wamekuwa wakitumia kemikali ambazo si salama zenye madhara kwa binadamu” anasema mdau wa mkutano huo Stephen Kijazi.

Hata hivyo pamoja na wakulima wengi kutegemea maji yatokanayo na mifereji inayotiririsha maji kutoka viwandani au sehemu isiyo salama kama kwenye makazi ya watu, bado elimu inatakiwa kwa wakulima hao hasa katika miji mikubwa nchini yenye viwanda kama Dar Es Salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza nk ili kuangalia ushirikwaji wao na waweze kutumia maji salama yanayotoka sehemu salama.

Merius Nzalawahe ni Afisa kilimo mkuu wa mazao ya bustani nchini kutoka wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi, pamoja na kushugulikia mazao ya bustani na mimeo inayohusiana na Afya za binadamu anasema; “mbogamboga ni vyakula muhimu sana kwa afya ya katika kuimarisha afya ya mlaji lakini pia mzalishaji anapozalisha mazao ya ziada umuongezea kipato, pia mazao haya yanapouzwa nje ya nchi yanaongeza uchumi wa taifa.”  

Vinginevyo ukulima wa mzao hayo unaolimwa pembezeni mwa barabara ambapo magari yanapita unamadhara kutokana na moshi wa magari unatoka na kuingia kwenye mimeo hiyo kuwa na madini yanayoleta athali kwa Afyaya binadamu. Hivyo basi ni nasafi kwa kila mkulima anayelima aina zote za mbogamboga kufuata kanuni bora za uzalishaji ili kutoa mazao yenye usalama kwa watumiaji.

Post a Comment

 
Top