0
Eneo ambalo ndege imeanguka kama linavyoonekana kwenye ramani.

Usafiri wa anga kwa kutumia ndege unasemekana kuwa ndiyo usafiri wenye usalama kuliko usafiri mwingine duniani, wakati huo huo baadhi wa wadadisi wanasema usafiri huo unaongoza kwa kuua watu wengi japo kuna wakati hautolewi taarifa zake kama ilivyo kwa vyombo vingine vya usafiri dunia.

Ndege iliyokuwa ikitokea Bolivia ilikuwa na watu 81 miongoni mwao ni wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense ya nchini Brazil imeanguka nchini Colombia katika eneo la Medellin, ambapo inadaiwa ilipata hitilafu katika mfumo wake wa umeme, taarifa zinasema watu 25 wamethibitishwa kufariki na wengine 6 wamenusurika katika ajali hiyo.

Ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa, iliwabeba wachezaji wa timu ya, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico National ambapo mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo kubwa  katika mashindano Amerika Kusini, ilikuwa imepangiwa kuchezwa Jumatano, lakini mpaka sasa imesitishwa.


Baadhi ya wachezaji ambao wanasemekana kufariki katika ajali hiyo ya ndege.

Timu hito inayotoka mji wa Chapeco, kusini mwa Brazil, ilipandishwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainali ya kombe hilo la Sudamericana kwa kuilaza San Lorenzo ya Argentina. Maafisa wa klabu hiyo ya Chapecoense wametoa taarifa wakisema: "Tunamuomba Mungu awe na wachezaji, maafisa, wanahabari na wageni wengine watu ambao walikuwa wameandamana na ujumbe wetu."


Post a Comment

 
Top