Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya
habari ambao wamehudhulia mafunzo hayo katika hoteli ya Holiday Inn
wakifuatilia mafunzo hayo mapema leo jijini Dar Es Salaam.
|
Kulia ni Profesa Rutinwa kutoka chuo kikuu
anayeangalia simu kushoto kwake ni Nondo Nobel
Bwami mratibu wa jamii ya wakimbizi wa shirika la Asylum access Tanzania.
|
HABARI KWA UNDANI
Leonard Mutani.
Mafunzo kwa
wanahabari juu ya mchango wao katika utetezi wa haki za wakimbizi, maisha na
uhalisia wa wakimbizi nchini na kimataifa, yametolewa na shirika la ASYLUM
ACCESSS la jijini Dar Es Salaam likiwa na lengo la kuwafanya wanahabari waweze
kuwa na uelewa mpana unaohusu wakimbizi.
Mikataba juu ya
wakimbizi imekuwa ni tatizo huku wakimbizi wengi wakikosa namna ya kufanikisha
malengo yako kutokana na kujua au kutojua wafanye nini wanapokuwa nchi tofauti
na ile aliyozaliwa. Wakati mwingine vigezo vinavyomfanya mtu kuwa mkimbizi katika
taifa lolote duniani ni vile ambayo vinatokana na chi husika ambapo inakuwa ni
tofauti na zile za kimataifa.
Mikataba ya haki za
binadamu
inahusisha kanuni mbalimbali za uhifadhi ambazo zinalenga kumfanya raia anayetaka
ukimbizi azifuate, japo kuna ubaguzi huu kwa upande mwingine unatokana na
baadhi ya raia wa nchi aliyokimbilia kutokuwa na uelewa juu ya mkimbizi. Vilevile
ulinzi
na haki kwa mkimbizi
ni sehemu mojawapo ambapo wakati kunapotokea mtu yeyote anakwenda kwenye nchi
isiyo yake anapaswa kupewa ili kumuondosha katika hofu na adha.
Katika mfumo wa
kawaida wa maisha mtu yeyote anayepatwa na majanga akiwa nchini kwake na
kuikimbia nchi yake kwa madhumuni ya kuhitaji uhifadhi aitha kutokana na vita ana
haki ya kupatiwa uhifadhi kwa nchi anayotaka kupata uhifadhi, hata hivyo mtu
yeyote hapaswi kupewa hifadhi kutokana na mambo ya kisiasa kama yale yanahohusu
kuleta vita au maafa katika nchi yake.
Hayo ni baadhi ya mafunzo yaliyotolewa
katika kumpa mwandishi wa habari nafasi ya uelewa kitaifa na kimataifa jinsi
sheria zinavyomruhusu mkimbizi kufanya kazi kwa sasa pasipo kuwa na USD 2000
ikiwa ni sehemu ya uboleshwaji wa sheria za wakimbizi kupata ajira nchini.
Post a Comment