Rais mteule wa Marekani
Donald Trump
|
Rais mteule wa Marekani
Donald Trump amesema haoni faida ya kulipwa kulipwa mshahara wa Rais wa USD$ 400,000
ambazo ni zaidi ya Tshs 872000000 atakapochukua hatamu rasmi akiwa katika ikulu
ya White house hapo Januari mwakani.
Kutokana na hatua ya
mteule huyo wa taifa hilo kubwa duniani kiuchumi na linalosadikiwa kuwa lenye
nguvu, badala yake anatarajia kulipwa kiasi cha USD $1 sawa na fedha ya
kitanzania 2180/- tu kwa kila mwaka.
Bwana Trump alifichua siri hiyo pale alipokuwa akifanya
mahojiano na mwandishi wa kituo cha CBS NEWS
Lesley Stahl wakati wa kipindi kilichochukua dakika 60.
Pamoja na kutojua anapaswa kulipwa kiasi gani cha pesa, Bw Trump alisema anadhani anahitaji kuchukua
USD $ 1 tu. Hata hivyo mwandishi huyo Bi Stahl alipomjulisha kwamba mshahara anaopaswa
kulipwa Rais ni USD $400,000, Bwana Trupm alisema:
"Hapana, sitaupokea mshahara huo na sizichukui kamwe."
Kutokana na hatua hiyo inawezekana Bw. Trump kuwa
ndiye Kiongozi wa kwanza kukataa mshahara mnono kama huo? Hapana, inasemekana hapo
nyuma kumekuwepo na viongozi kadhaa ambao waliwahi kuacha kuchukua mshahara wao
kutokana na sababu walizozifaham wao, mfano Herbert
Hoover, aliyekuwa ni tajiri kutokana na biashara ya madini ikiwa ni kabla ya kuingia
madarakani, mwingine ni John F Kennedy yeye alirithi utajiri, wote hao walikataa
kupokea mashahara na badala yake wakatoa pesa hizo zisaidie watoto wenye uhitaji
na watu wasiojiweza katika jamii.
Habari ni kwa msaada wa vyombo vya habari vya kimataifa.
Post a Comment