Leonard Mutani.
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Chuo cha utumishi wa
umma nchini tawi la Mtwara (TPSC) kimefanya mahafari ya 25 huku ikikusanya
wahitimu kutoka mikoa mitano (5) nchini yenye
matawi ya chuo hicho ikiwemo, Dar es salaam, Mbeya, Tabora, Singida, Tanga na ikiwemo
na Mtwara ambao kwa mwaka huu umechukua jukumu la kufanikisha sherehe za
mahafari hayo.
Katika mahafari hayo ambayo Mh. Angellah Kairuki
naibu waziri ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa umma na utawala bora, katika
yaliyofanika katika viwanja vya mashujaa mkoani mtwara, yaliudhuliwa na
wahitimu wapatao zaidi ya 800 huku wahitimu 2380 wakihitimu mafunzo mbalimbali
katika tasnia tofauti.
|
PICHA: Wahitimu wakiwa katika maandamano kutokea ofisi za mkuu wa mkoa wa Mtwara kuelekea viwanja vya mashujaa. |
|
PICHA: Naibu waziri ofisi ya Rais ofisi ya menejiment utumishi wa umma Angellah Kairuki (katikati) mwenye Joho rangi nyekundu akiwa na baaddhi ya waadhili wa vyuo vya utumishi wa umma nchini wakielekea kuwapokea wahitimu, hawapo pichani. |
|
PICHA: Naibu waziri mwenye Joho rangi nyekundu akiwaongoza wahitimu mara baada ya kuwapokea kueleke sehemu maalum kwa ajili ya kutunukiwa ngazi tofauti za elimu/kozi wakiwa katika maandamano ya pamoja. |
|
PICHA: Wahitimu wakiwa wameketi wakisikiliza na kusubili wakati muafaka kutunukiwa vyeti, diploma nk katika viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara.
|
PICHA: Baadhi ya wahitimu kutoka Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutunukiwa vyeti na doploma zao.
PICHA: Kikundi cha sarakasi kutoka kundi la Mundu Group cha mjini Mtwara wakiburudisha na kuonyesha ujuzi mbele ya wahitimu na waalikwa wakati wa sherehe za mahafari ya wahitimu wa Chuo cha utumushi wa umma katika viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara.
Katika maafari hayo, zaidi ya wahitimu 65 walifaulu vizuri huku wakipata wastani wa GPA 3.50 na 4.80 huku jinsia ya kike ikionekana kuwa juu wakati ufauru ukionekana kuwa wa Daraja A ambalo ni Daraja la Kwanza ni mkubwa kwa Ordinary Diploma in Secretarial Studies kulinganisha matokeo ya mengine.
|
PICHA: Naibu waziri ofisi ya Rais..., Angellah Kairuki katikati akifuatilia kwa makini kila tukio kabla ya kuanza kutunuku vyeti na shahada kwa wahitimu kmbalimbali.
PICHA: Mmoja kati wahitimu ambaye mapema jina lake halikupatina ambaye ndiye anaongoza katika ufaulu kwa mwaka huu akitunukuwa na mh Naibu Waziri wakati wa hafla hiyo mkoani Mtwara.
|
PICHA: Baadhi ya wahitimu walioshika nafasi za juu katika ufaulu (Best Students) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri..., Angellah Kairuki na baadhi ya waadhili wa chuo cha utumishi wa umma nchini. |
|
Post a Comment