Taasisi ya Lumumba
Alliance Club of Tanzania imetoa tamko juu ya wote ambao wanatumiwa na mabeberu
ili kuvuruga urithi mkuu tulioachiwa na waasisi wa Taifa letu ambao ni AMANI, UMOJA na UDUGU WA KITAIFA.
Wakati nia na madhumuni
ya taasisi hiyo ya Lumuba Alliance Club of Tanzania ni kufanikisha nia njema,
maelewano, Amani , maendeleo kwa jamii na kupambana na umaskini, mkuu wa idara
ya fedha ndg Mohamed Hussein alitanabaisha taasisi hiyo kutokukaa kimya huku
kukitokea watanzania wachahe wanaotumiwa na mafisadi kutaka kuwatenganisha na
watanzania na kuharibu nia njema ya kuleta nabadiriko ya kiuchumi ikiwepo nidhamu katikautumishi wa Umma
yanayofanywa na Mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dr. john pombe
magufuri.
Pamoja na kupinga kauli
za uchochezi zinazotolewa ndugu Mohammed alinukuu mmoja wa wanasiasa amabye alitoa
kauli inayoonesha wakati wa mfumo wa chama kimoja ambapo hayati baba wa taifa
mwalimu Nyerere toka mwaka 1961 hadi 1962 ambapo kulikuwa na majaribio manne ya
kumpindua.
Hata LAC inawaomba
watanzania wote kwa umoja kulaani kitendo cha baadhi ya makundi hayo huku
akigusia lengo la serikali kuhamia Dodoma ambapo amegusia jinsi lengo la
kuamisha makao makuu ya nchi na huduma za kiserikali tangu 1973 TANU ilipoanza
mchakato kupitia balaza kuu, ambapo tayari baadhi ya ofisi za kiserikali zipo
tayari ikiwa na
baadhi ya watumishi kupewa fedha za uhamisho japo baadaye walirudi Dar Es
Salaam.
Aitha alihoji kauli
mbalimbali zinazotolewa na mheshimiwa Rais Magufuri ikiwa ni pamoja na kuwa
mkali kuhusu maliasili na utajiri wan chi yetu je, ni Udikteta? Na kuwataka
watanzania kujivunia Utaifa na Tanzania haitajengwa nan chi nyingine yoyote
bali itajengwa na watanzania wazalendo watakaojitoa mhanga kwa ajili ya
Tanzania.
Ni jambo jema kwa taasisi ya lumumba aliance club kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na serekali
ReplyDeleteNi jambo jema kwa taasisi ya lumumba aliance club kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na serekali
ReplyDeleteKweli LAC imeonesha Umoja wa kitaifa kwa maslahi ya wengi.
ReplyDelete