ARUSHA.
Chama wa
wanasheria nchini (Tanganyika Laws Society), kimefanya mkutano wake
wa mwaka na kufanya uchaguzi wa Rais wa chama hicho ambaye uchaguliwa kila
baada ya mwaka mmoja.
Kiti hicho cha Urais wa TLS hapo kabla kilikuwa kikishikiliwa na
mwanansheria Tundu Lissu ambaye kwa mujibu wa sheria amemaliza kipindi chake
pamoja na kuwa katika matibabu nchini Uberigiji.
Hapa chini ni baadhi ya picha za matukio ya kuapishwa kwa Rais
mpya wa chama hicho, mwanasheria Fatuma Karume, aliyechaguliwa katika mkutano
uliofanyika jijini Arusha.
PHOTO:
Mwanasheria Fatuma Karume akivishwa joho la kuchukua kiti cha Rais wa Chama cha
Wanasheria wa Tanganyika.
|
PHOTO: Rais wa
TLS Fatuma Karume (kulia) akiapa kuwa Rais wa TLS, pembeni kwake ni mwanasheria
Ngaro aliyesimamia zoezi hilo.
|
PHOTO: Rais akitoa shukurani kwa wanachama kumpa nafasi ya kuongoza chama chao mara baada ya kuapa.
|
PHOTO: Rais akiongea
na wanachama wa TLS hawapo pichani mara baada ya kuapishwa na kuchukua nafasi
hiyo majira ya jioni ya leo jijini Arusha.
|
PHOTO: Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Fatuma Karume akiwapungia mkono wanachama ambapo aliharisha mkutano huo mpaka mwakani kwa mkutano mkuu mwwingine.
|
Post a Comment