Mtu wa kwanza duniani kupandikizwa nyuso mbili
amesema kuwa anahisi vyema kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji na
kuwekewa uso alionao sasa, mtu huyo ajulikanaye kwa jina la Jerome
Hamon alitolewa uso huo mwaka uliopita baada ya kupata ishara za kukataliwa
kufuatia matibabu ya dawa ya antibiotic wakati aliposhikwa na homa.
Mtu
huyo mwenye umri wa miaka 43 aliendelea kuwepo hospitalini jijini Paris bila
uso wa kawaida kwa muda wa miezi miwili huku mfadhili akitafutwa mfadhili kwa
ajili ya matibabu hayo, kutokana na kuugua ugonjwa unaosababisha uvimbe kwenye
uso. Uso wake wa kwanza aliukublai mara moja, Hamone alisema,
Upandikizaji
wa uso huo ulifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2010 ambapo ulifanikiwa, lakini
akaambukizwa homa mnamo 2015 na kupewa dawa za antibiotics. Dawa hiyo
haikuingiliana na matibabu yake hatua iliosababisha damu yake kuukataa uso huo.
Ishara
za kwanza za uso huo kukataliwa na damu zilianza kufichuka mwaka 2016 na
Novemba mwaka jana ambapo ilibidi uso huo kuondolewa.
Hamon
aliishi bila uso katia chumba kimoja katika hospitali ya Groges-Pompidou mjini
Paris bila kuwa na uwezo wa kuona, kuzungumza ama hata kusikia hadi mwezi
Januari wakati ambapo mfadhili wa uso wake alipatikana na upandikizaji wa pili
kufanywa.
Ili
kuzuia uso huo kukataliwa na damu yake, bwana hamon aliyepewa jina Mtu mwenye
'nyuso tatu' na vyombo vya habari vya Ufaransa alipatiwa matibabu maalum
kusaficha damu kabla ya upasuaji huo kufanyika.
Uso
wake wa tatu ni mzuri ijapokuwa fuvu lake la kichwa , ngozi na vipengee vyake
havijaingiliana vyema. lakini anaamini kwamba atapona.
''Iwapo ningekataa uso
huu mpya ingekuwa vibaya sana, ni swala la utambulizi, lakini sasa tumefanikiwa
ni vyema kwangu'', aliambia chombo cha habari cha AFP
kutoka hospitali ambapo anaendelea kujiuguza.
''Mimi nina umri wa
miaka 43 na mfadhili wangu ana miaka 22 kwa hivyo nimerudi kuwa na miaka 22'', aliambia runinga ya Ufaransa.
Upuasiji
huo uliochukua saa kadhaa uliongozwa na Profesa Laurent Lantieri , mtaalamu wa
upandikizaji wa uso na mikono ambaye alimfanyia upasuaji wa kwanza bwana Hamon
miaka minane iliopita.
''Leo tunajua kwamba
upandikizaji wa nyuso mbili unawezekana , hauko tena katika taaluma ya
utafiti'', aliambia gazeti la Le Parisien
Daktari
Bernard Cholley alisema: Mtu yeyote anapopoteza uso wake na baadaye analazimika
kusubiri upandikizaji kwa muda usiojulikana hicho ni kitu ambacho hakuna mtu
amewahi kufanyiwa. Nimeshangazwa
na ujasiri wa mgonjwa ambaye ameweza kupitia matatizo haya. Upandikizaji wa
kwanza wa uso ulifanyika 2005 kaskazini mwa Ufaransa .
Source: BBC
Post a Comment